Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imempiga faini
ya sh. milioni moja na kumfungia miezi mitatu kocha wa makipa wa timu ya
Coastal Union kwa kuwatukana washabiki wanaominika kuwa wa Simba.
Pondamali
alifanya kosa hilo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya
timu yake na Yanga iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na
kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mwamuzi
Martin Saanya na mwamuzi msaidizi namba moja Jesse Erasmo waliochezesha
mechi kati ya Yanga na Coastal Union nao wamefungiwa mwaka mmoja kila
mmoja kwa kutoimudu mechi hiyo.
Nayo
Yanga imepigwa faini ya sh. milioni moja (sh. 500,000) kwa kila kosa
kutokana na washabiki wake kuwarushia waamuzi chupa za maji baada ya
Coastal Union kusawazisha bao katika mechi hiyo. Pia waliwarushia chupa
waamuzi hao wakati wakirejea vyumbani baada ya pambano hilo.
Vilevile
Coastal Union imepigwa faini ya sh. 100,000 baada ya kuchelewa kwenye
kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting). Timu hiyo ilichelewa
kwa dakika 23. Kikao kinatakiwa kuanza saa 4 kamili asubuhi.
No comments:
Post a Comment