Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Mwanzilishi na Mkurugenzi waShirika la Africa
School House Bi.Ainee Bessire (watatu kushoto) pamoja naMbunge wa
Misungwi Charles Kitwangwa(kushoto) na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia
Evarist Ndikilo(kulia) wakikata utepe kuzindua rasmi shule ya msingi
Ntulya katika kata ya Mondo wilayani Misungwi.Shule hiyo imejengwa kwa
msaada wa Shirika lisilo la kiserikali la Africa School House lenye
makao yake nchini Marekani.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi
mkoani Mwanza ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya
msingi Ntulya muda mfupi baada ya kuizindua katika kata ya Mondo
wilayani Misungwi leo. Shule hiyo imejengwa kwa msaada wa Shirika lisilo
la kiserikali la Africa School House lenye makao yake nchini
Marekani.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza ambapo
atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo. Picha na Freddy Maro
************************************
************************************
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Septemba 6,
2013, amefungua shule ya kisasa ya msingi ya Ntulya katika kata ya Mondo,
Wilaya ya Misungwi, iliyotolewa kama zawadi kwa wanakijiji cha Ntulya na
taasisi moja ya Marekani.
Aidha, Rais Kikwete
amezindua huduma za x-ray kwenye Hospitali ya Wilaya ya Misungwi mjini Misungwi
ikiwa ni hatua zake za mwanzo kwenye siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Rais
Kikwete katika mkoa wa Mwanza ambako atakaa siku tano akikagua na kuzindua
miradi na shughuli za maendeleo.
Shule ya Ntulya
iliyoko kilomita 47 kutoka mjini Misungwi ina wanafunzi 466 na walimu 11 na ni
zawadi ya Taasisi ya Africa School House ya Marekani kwa wanakijiji cha Ntulya
ambako Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt. Aimee Bessire ambaye
amehudhuria sherehe za uzinduzi wa shule hiyo na mume wake, Mark Bessire
walipata kuishi wakifanya utafiti kuhusu utamaduni wa Kabila la Wasukuma.
Shule hiyo ya kisasa
imejengwa kwa matofali ya kuchomwa na ilijengwa kati ya 2008 na 2010. Ina
madarasa 11, nyumba 10 za walimu na kisima cha maji safi. Kwa jumla shule hiyo
ina uwezo wa kuwa na wanafunzi 600 kwa wakati mmoja.
Akizungumza kwenye
sherehe za leo, Dkt. Bessire ambaye amezungumza kwa ufasaha lugha za Kiingereza,
Kiswahili na Kisukuma, amesema kuwa shule hiyo imejengwa kwa jumla ya sh
bilioni 1.038, na kati ya hizo sh milioni 980 zilitolewa na Africa School
House, Halmashauri ya Misungwi ilichangia sh milioni 28 na nguvu za wananchi
zilichangia sh milioni 30.
Taasisi hiyo ya
Marekani pia imewajengea wanakijiji hao wa Ntulya Kituo cha Afya kwenye eneo
hilo la shule na Dkt. Bessire amesema kuwa Taasisi hiyo ina mipango ya kujenga
shule ya mfano ya sekondari ya bweni ya wasichana.
Dkt. Bessire pia
amesema kuwa yataanzishwa madarasa kwenye shule hiyo kwa ajili ya watu wazima
wasiojua kusoma na kuandika.
No comments:
Post a Comment