Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a akitoa baadhi ya maelekezo kwa
nahodha wa Boti mara baada ya kuanza safari kuelekea katika Kijiji cha
Kipwa mwambao mwa ziwa Tanganyika kwa ajili ya kuwatembelea na kuwapa
pole wahanga wa ajali mbaya ya kwanza kuwahi kutokea katika Kijiji
hicho. Ajali hiyo ya Boti inayodaiwa kusababishwa na hali mbaya ya hewa
katika ziwa hilo ilipelekea vifo vya watoto 11 na kinamama wawili. Mtoto
mmoja na mama mmoja kati yao ni raia wa nchi jirani ya Zambia na tayari
walishapelekwa nchini kwao kwa ajili ya taratibu za maziko. Abiria
walookoelewa na kunusurika katika ajali hiyo ni 15 wakiwepo wakinamama
13 na watoto wawili, dereva wa boti hiyo mpaka msafara wa Mkuu wa Wilaya
unaondoka kijijini hapo hakufahamika alipo. Abiria hao
walikuwa wanatoka katika kijiji cha jirani cha Kapele kufata Zahanati
kwa ajili ya chanjo, wakiwa njiani ndio wakapatwa na msiba huo.
Muongozaji
Mkuu wa Blogu ya Rukwareview Hamza Temba hakuwa nyuma kuhakikisha tukio
hili zima linaruka hewani, hapo life jacket na kipenga mfukoni chochote
kinaweza kutokea; Usalama Kwanza. "...tunashukuru Mungu tulienda salama
na kurudi salama..."
Kijiji
cha Kipwa kinavyoonekana kutokea ziwani (Tanganyika). Mpasuko wa milima
unaoonekana ni kilele cha bonde na mto Kalambo (Kalambo Falls).
Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a akimpa pole Ndugu Hassan Abdul
ambaye ni mmoja wa wafiwa katika ajali hiyo mbaya ya boti ilyoua watoto
11 na kinamama wawili. Ofisi ya Wilaya ya Kalambo kwa kushirikiana na
Chama Tawala (CCM) ilitoa ubani wa Tsh. 90,000/= kwa kila kaya
iliyopatwa na msiba huo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a akiwa amemshikilia mtoto Prisila
Skapite (7) aliyefanikiwa kujiokoa katika ajali hiyo kwa kuogelea na
kipande cha ubao hadi nchi kavu, mdogo wake aliyemshikilia alifanikiwa
kuokolewa pia katika ajali hiyo.
Mama
Roza Zunda naye alifanikiwa kujiokoa na mtoto wake kwa kumshikilia kama
inavyoonekana pichani huku akiwa ameshikilia gunia la
sabuni lililomsaidia kuogelea hadi nchi kavu na kuookolewa na waokoaji
kutoka kijiji cha Kipwa baada ya kuishiwa nguvu.
Mkuu
wa Wilaya ya Kalambo ambaye pia alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Injinia Stella Manyanya akiongea na wananchi wa kijiji cha Kipwa
kilichopo mwambao wa Ziwa Tanganyika na kuwapa rambirambi za Serikali
ambapo pia aliahidi kurudi katika kijiji hicho kufanya mikutano ya
hadhara. Aliahidi kuwa Serikali itasaidia kujenga kituo cha afya katika
kijiji hicho pamoja na kufuatilia ujenzi wa barabara itakayosaidia
kuunganisha kijiji hicho na maeneo mengine ya Mkoa kutokana na ukweli
kwamba kwa sasa ijiji hicho kinafikika kwa njia ya maji peke yake kwa
kutumia Boti.
Afsa
Mkuu wa SUMATRA Mkoa wa Rukwa (kulia) akiwa na DSO Wilaya ya Kalambo
wakirudi kutoka katika Kijiji cha Kipwa kwa Boti mara baada ya
kutembelea wahanga wa ajali hiyo mbaya ambayo haijawahi kutokea katika
kijiji hicho.
Safari ya kurudi.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
No comments:
Post a Comment