skip to main |
skip to sidebar
SERIKALI YAMPONGEZA MZEE GURUMO
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Utamaduni, Bibi. Lilly Beleko kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo akimkabidhi Mzee Muhidini Gurumo barua kama ishara ya
Serikali kutambua mchango wake uliotukuka katika tasnia ya Muziki nchini
pamoja na kumpongeza kwa kustaafu kazi kazi hiyo, hivi karibuni
nyumbani kwake Makuburi, Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia nyuma ya
Mkurugenzi ni Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Bw. Addo Mwasongwe
na kulia pembeni ya Mzee Gurumo ni Mkewe, Bibi. Pili Said Kitwana.
Nguli wa Muziki wa Dansi, Mzee
Muhudini Gurumo (aliyevaa shati la drafti) akiwa na watumishi wa Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, walipomtembelea nyumbani kwake
Makuburi Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Serikali kupitia Wizara
hiyo ilimkabidhi barua rasmi Mzee huyo kutambua mchango wake katika
tasnia ya Muziki na kumpongeza kwa kustaafu kazi hiyo. Wa kwanza kulia
ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Bibi Lilly Beleko, wa
pili ni mke wa Mzee Gurumo, Bibi. Pili Said Kitwana na wa Pili Kushoto
ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara Upande wa Sanaa, Bibi. Joyce
Hagu.
Picha zote na Concilia Niyibitanga
No comments:
Post a Comment