Nipo hapa Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda.....siamini ninachokiona machoni mwangu....kuanzia jana tarehe 1/09/2013 serekali ya Rwanda imeongeza ushuru wa barabara ( ROAD TOLL) kwa magari yote ya Mizigo ( Fuel and Dry Cargo) yenye plate numbers za Tanzania kutoka USD 152 mpaka USD 500 kwa kila gari.
Kwa taarifa ambazo sio rasmi kwa siku magari ya mizigo takribani 300 yanavuka hapa mpakani, na zaidi ya asilimia 95% ya magari hayo zina plate numbers za Tanzania.
Wanajamii hii ina madhara gani kwa uchumi wa Tanzania kwani akili ya harakaharaka hii ni some sort of Protectionism ila kwa mbali inaweza ikawa ni muendelezo wa chokochoko.
No comments:
Post a Comment