Mwandishi
wa Habari wa kujitegemea mkoani Singida wa Magazeti ya Mwananchi
Communications Limited, Awila Silla akiwa wodini katika Hospitali ya
Mkoa wa Singida, baada ya kupigwa mapanga na mtu asiyejulikana Jumapili
iliyopita, mwaka huu, mjini Singida. Picha na Gasper Andrew.
Mwandishi wa Habari wa kujitegemea wa Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti mkoani Singida, Awila Silla amejeruhiwa baada ya kukatwa na mapanga kichwani na mtu asiyejulikana.
Tukio hilo lilitokea juzi saa 2 usiku
Jumapili iliyopita maeneo ya Utemini ambapo alivamiwa na mtu huyo ambao
mbali na kumjeruhi kwa mapanga, pia alimpiga ngumi na mateke na
kumjeruhi katika jicho lake la kushoto.
Silla amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Singida ambapo alifikishwa na kijana mmoja (jina halikumbuki) ambaye
alimkuta akiwa hajitambui.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa,
Geofrey Kamwela alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kuwa hana taarifa
yoyote na kuahidi kuwa atafuatilia tukio hilo.
Silla ni mwakilishi wa gazeti hili mkoani humo na huandika zaidi Makala za kijamii na kiutamaduni.
Tangu afikishwe katika hospitali hiyo, watu
mbalimbali walikwenda kumjulia hali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk
Parseko Kone.
Akisimulia mkasa huo akiwa hospitalini,
Silla alisema, nilikuwa nikirejea nyumbani muda ya jioni nilipofika
maeneo ya Utemini simu yake ya kiganjani ikaita na kulazimika kuzungumza
ghafla akatokea kijana ambaye alikuwa amejifunika shuka la kimasai na
kuanza kumfuata.
“Nilipogundua yule kijana ananifuata kwa
kasi nikaongeza mwendo lakini kila nilipojaribu kumkwepa alizidi
kunifuata mpaka nilipofika karibu na uzio wa nyumba moja akanikaribia na
kuanza kunivamia kisha kunibamiza katika geti la nyumba hiyo.”
Alisema baada ya kufanikiwa kunidhibiti
akaanza kunicharanga na mapanga huku akidai nimpatie pesa, nikamwambia
sina pesa lakini cha kushangaza akasema wewe huwa una hela.
“Alinishangaza sana, inaonekana kama
ananijua, lakini kila nilipokuwa namkaribia ili nimjue vizuri alikuwa
anazidi kunisukuma nisimgundue.”
Kwa mujibu wa Silla, mtu huyo
alimnyang’anya simu pamoja na mfuko uliokuwa na vifaa vidogo ambavyo
alitoka kununua yakiwamo mafuta.
mwananchi
No comments:
Post a Comment