JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO
YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI
TANZANIA
PRESS RELEASE
11/09/2013
Kujeruhi kwa
risasi: - Tarehe 10/09/2013, saa 6:30 mchana huko Kijiji Tondoroni (W) Kisarawe (M) Pwani.
Omary S/o Mohamed, umri miaka 47, fundi ujenzi, mkazi wa Tondoroni Kisarawe
alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni wa kulia na watu wanaosadikiwa kuwa ni
askari wa JWTZ kikosi 83 Kiluvya wakati akiendelea na shughuli zake za ujenzi.
Chanzo ni madai ya mlalamikaji kujenga katika eneo linalodaiwa ni la Jeshi.
Taarifa ya
Kifo. Tarehe 10/09/2013 majira ya 01:20 usiku huko Mbegani katika bahari ya
Hindi Kata ya Zinga (W) Bagamoyo (M)
Pwani Watu wapatao sita wakiwa wanasafiri na Boti ijulikanayo kwa jina la GOGO
WATER BOAT mali ya Lazy Lagon Lodge wakitokea Mbegani wakielekea kwenye Kisiwa Las Lagon walizama majini na kusababisha vifo
kwa (1) Elikulano S/o Malile, 39 yrs, mlinzi wa hoteli hiyo na(2) Mwanahawa D/o Mtungi, 30 yrs, mkulima watu wawili walifanikiwa kuopolewa
ambao ni Levina S/o Mdemu, 29 yrs,
nahodha wa Boti na (2) Daudi S/o
Kiando, 32 yrs, Fundi injini na
mfanyakazi wa hoteli hiyo, ambao
hawajapatikana ni (1) Robert S/o Kambo,
34 yrs, Kapteni wa Boti, (2) Elisando
S/o Malile, miezi minne (4) , mtoto wa Mwanahawa D/o Mtungi. Chanzo cha ni kuchafuka kwa
bahari. Juhudi za kuwatafuta waliozama
bado zinaendelea.
Taarifa ya
kifo: - Tarehe 10/09/2013, saa 10:10 jioni katika Kijiji cha Kiromo (W)
Bagamoyo (M) Pwani. Mohamed Iddi umri miaka 9, mkazi wa Kiromo Miono aliangukiwa
na mnazi uliokuwa umekauka kichwani na kupasuka fuvu la kichwa wakati wakiwa
machungani na wenzake na kufariki papo hapo. Mnazi huo ulikuwa umekauka na
mizizi yake kuoza hivyo upepo ulipovuma ndipo ukadondoka na kumwangukia
marehemu. Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu kwa
mazishi.
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA PWANI

No comments:
Post a Comment