Ni habari njema zilizoeneza zaidi ya wiki tatu zilizopita kuhusu show
mpya ya TV ambayo inaongozwa na mwigizaji Mtanzania Irene Uwoya.
Irene kupitia AMPLIFAYA ya Clouds FM alitangaza kuacha kuigiza movie na
sasa atawekeza muda wake kwenye show ya TV ambayo imelenga kukarabati
nyumba mbovu za Watanzania.
Utaratibu anaoutumia ni kupokea maombi ya Watanzania wanaohitaji nyumba
zao kukarabatiwa alafu Irene na timu yake ndio wanachagua nyumba ya
kuikarabati, huduma ambayo wanaitoa bure….
Hii video hapa chini ni sehemu ya mfululizo wa show ya Irene Uwoya ambayo inaonekana @Clouds_TV peke yake.
No comments:
Post a Comment