Pages

Thursday, September 19, 2013

TIC kuendelea kuwawezesha wajasiriamali kukidhi viwango vya kimataifa



Afisa Mwandamizi Huduma kwa Wawekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Bw. Patrick Chove akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) umuhimu wa wananchi kushirikiana na wawekezaji katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Kaimu Meneja wa Tafiti na Mipango wa Kituo hicho Bw. Njoki Tibenda.

Meneja Mawasiliano wa Kituo cha Uwekezaji Bi. Pendo Gondwe (kulia) akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafuzo ya kitaalam waliyoyatoa  kwa wajasiriamali 285 katika Mikoa ya Dar es Salaam,Kilimanjaro, Mwanza na Mbeya ili kuwawezesha kukabiliana na ushindani wa kiuwekezaji na kufikia viwango vya kimataifa, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Afisa Mwandamizi Huduma kwa Wawekezaji Kituo hicho Bw. Patrick Chove.
(Picha na Hassan Silayo)



OFISI YA WAZIRI MKUU
KITUO CHA UWEKEZAJI
Kituo cha Uwekezaji  Tanzania TIC kinapenda kutoa taarifa kwa Umma kuhusu mafanikio ya Mpango wa kuwaunganisha Wajasiriamali wadogo na wakati (Business Linkage)na Makampuni Makubwa ya kigeni (TNC’S)   na ya Kitanzania ambapo kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara (UNCTAD) Mpango huo wa kukuza Uwezo wa kibiashara kwa wajasiriamali kufanya biashara na Makampuni hayo makubwa.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ni moja Taasisi ya Serikali ilianzishwa chini ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania, Namba 26 ya mwaka 1997 kwa kuendeleza, kuratibu na kuwezesha uwekezaji katika Tanzania. Kama sehemu ya jukumu letu, TIC ina jukumu la kuhamasisha uwekezaji na masuala yanayohusiana na Uwekezaji kwa Watanzania ili Uwekezaji uweze kuwa na manufaa kwa Watanzania kwa ujumla.
Katika kipindi chote cha Mpango huo Watanzania wameweza kuongezewa uwezo kwa kupewa fursa mbalimbali za kiutalamu za kuweza kukabiliana na ushindani na kuwawezesha kufikia viwango vya Kimataifa vinavyohitajika na makampuni makubwa ili Makampuni hayo yaweze kutumia bidhaa za Kitanzania badala ya Kuagiza nje Bidhaa hizo.
Mpaka sasa kituo kimeweza kutoa mafunzo hayo ya Kitaalamu kwa WAJASILIAMALI wapatao 285 katika mikoa ya Dar-es-salaam, Kilimanjaro, Mwanza na Mbeya.
Katika Mafunzo hayo zaidi ya MAKAMPUNI MAKUBWA 28 yaliweza kuhusishwa  katika kuwajengea uwezo na kuwaongezea Utaalamu.
TIC pia katika jitihada zake za kuongeza faida za uwekezaji katika uchumi wa Tanzania pia walifanya shughuli kuu ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wawekezaji kupata vibali vyote vinavyohitajika chini ya One Stop Shop na utoaji wa huduma kwa wawekezaji aftercare.
TIC imeweza kusajili Miradi kadhaa na katika usajili huo inawasilisha sekta tano zinazoongoza katika kusajiliwa miradi katika kipindi cha Januari mpaka Juni 2013 ambazo ni sekta ya Uzalishaji viwandani miradi 138, Utalii miradi 115, Usafirishaji miradi 82 majengo ya biashara miradi 65 na kilimo miradi 23. Jumla ya miradi yote ilikuwa ni miradi 454 na matarajio yetu ni kuwa mwaka huu tutasajili miradi zaidi.
Katika usajili wa miradi hiyo wawekezaji wa nje waliweza kusajili miradi 120 , Miradi ya Ubia kati ya wageni na watanzania ilikuwa ni 92 na miradi ya Watanzania 242 ambayo ni zaidi ya nusu ya miradi yote.

No comments:

Post a Comment