Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati), akiitembeza na kuionyesha timu ya Serengeti Fiesta baadhi ya vitu vinavyofanyika shambani hapo.
Waziri
Mkuu akimfafanulia jambo Mkurugenzi wa Vipindi, Uzalishaji na Maendeleo
wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba (kulia), moja ya mikakati yake ya
baadaye atakayoifanya shambani hapo.
Mtalamu na msimamizi mkuu wa mashamba hayo aliyeshika chupa (kushoto), akionyesha moja ya chupa ya asali inayotengenezwa hapo.
Mtalamu wa mashamba hayo akiwatembeza na kuwapa maelezo na jinsi walivyoweza kufanikisha kilimo na ufugaji huo.
Mtangazaji wa Kipindi cha Jahazi, Wasiwasi Mwabulambo (kulia), akipokea zawadi ya zabibu kutoka kwa Waziri Mkuu.
Mwandishi wa Kampuni ya Global Publishers LTD, Musa Mateja (kushoto), akipeana mkono wa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
TIMU
ya Serengeti Fiesta hususani iliyoupande wa kampeni ya Kamata Fursa
Twenzetu, jana ilipata mwaliko kutoka kwa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo
Peter Pinda wa kutembelea katika mashamba yake.
Timu
hiyo ilifika kwenye mashamba hayo yaliyopo Kizota nje kidogo ya mji wa
Dodoma eneo la Zuzu ambalo ndilo jina halisi la mashamba hayo
yanayohusika na shughuli mbalimbali za kilimo, ikiwemo ufugaji wa mbuzi
zaidi ya mia mbili, kilimo cha zabibu, nyanya, ndizi na ufugaji wa
asali.
Timu hiyo ilikuwa ikiongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi, Uzalishaji na
Mipango wa Clouds Media Group, Rugemalila Mutahaba ‘Ruge’, ilipata fursa
ya kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa Waziri Mkuu, hasa kuhusiana na
namna ya kutumia fursa ya kujikwamua kimaisha kupitia kilimo na
ufugaji.
(HABARI/PICHA:MUSA MATEJA/GPL)
P
No comments:
Post a Comment