Thomas Ulimwengu alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na Samatta moja, wakati linguine lilifungwa na Tressor Mputu Mabi.
Ulimwengu aliifungia Mazembe bao la kwanza dakika ya nne kwa kichwa, ambalo halikudumu sana baada ya beki Mohamed Ziti kusawazisha dakika nne baadaye.
Mazembe ikazinduka na kupata bao la pili dakika ya 16 lililofungwa na Tessor Mputu, ambaye aliipangua safu ya ulinzi ya Setif na kumtungua kipa Sofiane Khedairia.
Ulimwengu akaifungia Mazembe la tatu dakika ya 27, akimalizia krosi maridadi ya Mbwana Samatta, ambaye alimtoka Abdelghani Demmou.
Mazembe ilipata bao la nne dakika ya nne baada ya kutimia saa moja mchezoni kupitia kwa Samatta, ambaye alitumia vizuri udhaifu wa beki Demmou.
Mputu alipata nafasi nzuri ya kufunga dakika tatu baadaye, lakini Khedaria akaokoa na Setif ikapata bao linguine dakika ya 71 kupitia kwa mshambuliaji wake, Kaled Gourmi, aliyemtungua vizuri kipa Robert Kidiaba.
Mazembe ilipewa penalti dakika za majeruhi, lakini kiungo Ngasanya Ilongo akapaisha.
Timu hiyo ya DRC sasa imetinga Nusu Fainali ikiwa bado ina mchezo mmoja mkononi, baada ya kutimiza pointi 10 kutokana na mechi tano.
FUS Rabat, ambayo itamaliza na Mazembe katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo B, inaweza kuungana na akina Samatta na Ulimwengu ikiwa itawafunga wenyeji CA Bizertin ugenini Tunisia leo. Bizertin na FUS zimefungana kwa pointi tano kikla moja. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment