Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
WAKATI
England wakihangaika kufuzu fainali za kombe la Dunia ingawa wamepumua
baada ya kupata suluhu ya bila kufungana na Ukraine usiku wa jana, kwa
Wabrazil mambo yanazidi kuwa barabara baada ya Neymar kuendelea kung`ara
na kikosi chake cha Timu ya Taifa kuashiria kuwa majira ya kiangazi
mwakani watakuwa wanasaka mwari wa kombe la Dunia.
Ndiyo,
ilikuwa mechi ya kirafiki tu dhidi ya Ureno yenye nyota wake Cristiano
Ronaldo, lakini Neymar mwenye umri wa miaka 21 ameonesha thamani yake
nyuma ya kivuli cha nyota mwenzake wa FC Barcelona, Lionel Messi baada
ya kuingoza Brazil kupata ushindi wa mabao 3-1.
Kikosi cha Brazil:
Julio Cesar, Maicon, Thiago Silva, Luiz, Maxwell, Paulinho (Henrique
83), Gustavo, Ramires (Oscar 61), Bernard (Hernanes 68), Jo (Pato 76), Neymar (Lucas Moura 89). Subs not used: Jefferson, Marcos Rocha, Fernando, Dante.
Aliyeoneshwa kadi: Neymar, Ramires.
Waliofunga mabao: Thiago Silva 24, Luiz, Neymar 34.
Kikosi
cha Ureno: Rui Patricio, Joao Pereira (Postiga 70), Pepe (Luis Neto
46), Bruno Alves, Fabio Coentrao (Antunes 54), Veloso, Vieirinha (Lica
84), Meireles, Joao Moutinho (Ruben Amorim 59), Nani, Nelson Oliveira.
Subs not used: Eduardo, Andre Martins, Ricardo Costa, Adrien Silva,
Josue, Lopes.
Waliooneshwa kadi: Pereira, Postiga, Bruno Alves.
Bao: Meireles 18.
Macho yote juu yangu: Neymar amewafanya kitu mbaya sana Ureno usiku wa jana huku akipiga goli matata
Hazuiliwi: Neymar na Brazil wanaonekana kuimarika zaidi
Furaha kinoma noma: Raul Meireles (kushoto) na Miguel Veloso (kulia) wakishangilia bao lao la kwanza
Muda wa shangwe: Ureno wakishangilia bao lao la kwanza ambalo likageuka kuwa la kufutia machozi
Cheki kitu cha ndosi: Thiago Silva akipaa hewani kumalizia kona iliyochongwa na Neymar na kupachika bao
Ooh! Mungu wangu: Nani (kulia) akijilaumu baada ya kupoteza nafasi ya kufunga
Mambo ya ndosi: Jo (watatu kushoto), aliyefunga bao la tatu akiosha mpira wa kona
No comments:
Post a Comment