Pages

Monday, September 30, 2013

Vijana wanavyosajiliwa kupigania Al Shabaab


alshabaab-soldiers-in-training_495033_e5a43.png
Uchunguzi wa BBC umefichua ambavyo vijana husajiliwa kujiunga na kundi la kigaidi la Al Shabaab katika pwani ya Kenya.
Al Shabaab limekiri kufanya shambulizi la kigaidi dhidi ya jengo la Westgate ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa na mamia kujeruhiwa.
Uchunguzi wa BBC, unatizama ambavyo vijana wanafunzwa itikadi kali za dini katika kuwaandaa, kujiunga na kundi la Al Shabaab
Vikao vya kuwasajili Vijana hao huanza na viongozi wa dini kutoa hotuba kwa vijana waisilamu wengi ambao wamesilimu.
Uchunguzi huo umebaini kuwa vijana hao ambao wanakuwa wamejitolea kupigania kile wanachosema ni dini, hupelekwa katika maeneo ya vijijini katika fuo za bahari kama sehemu ya kwanza ya safari yao kwenda Somalia.
Mmoja wa wahubiri hao kwa jina Makaburi, ametetea shambulizi lililofanywa dhidi ya Jumba la Westgate na kuwaua watu zaidi ya sitini akisema kwamba ilikuwa hatua sahihi.
Kulingana naye, ilikuwa sawa kwa sababu majeshi ya kigeni yanapigana nchini Somalia.
Jeshi la Kenya lilipeleka wanajeshi wake nchini Somalia,miaka miwili iliopita kupambana na kundi la Al Shabaab.
Wakati huohuo, maombi yanafanyika katika sehemu mbali mbali mjini Naiobi kuwaombea waathiriwa wa shambulizi hilo.

No comments:

Post a Comment