Waziri
Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kulia) akikata utepe leo kuashiria ufunguzi
wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China yanayofanyika
katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya
siku nne yanalengo la kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini humo ili
viwanda na makampuni ya nchi hiyo waweze kufanya biashara na watanzania.
Kulia kwa waziri mkuu ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah
Kigoda na kushoto kwake ni Balozi wa China nchini LV Youqing.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda alijaribu jembe la kupandia nafaka wakati
alipotembelea banda la kiwanda cha Qingyuan Manchu Autonomous County
cha nchini China wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini
humo yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam.Wanaomtazama ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda
(kushoto) na Balozi wa China nchini LV Youqing (kulia).
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akiangalia malighafi zinazotumiwa na kampuni ya
Beijing New Building Material kutengenezea nyumba alipotembelea banda
hilo leo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini
China yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam. Wa kwanza kushoto ni Meneja Msaidizi Idara ya Biashara ya
Kimataifa wa Kampuni hiyo Alec Lu na wapili kulia ni Makamu Meneja Mkuu
Fred Yu.
Mfanyakazi
wa kiwanda cha Changzhou Amec Group cha nchini China Yan Xing Long
(kulia) akimueleza Waziri Mkuu Mizengo Pinda jinsi mashine ya
kuchanganya kokoto iliyotengenezwa na kiwanda hicho inavyofanya kazi
wakati wa maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini humo yanayofanyika
katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akiangalia mfano wa nyumba zinazojengwa na kampuni
ya Beijing New Building Material alipotembelea banda hilo wakati wa
maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa nchini China yanayofanyika katika
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Waziri
wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda na watatu kushoto ni Meneja
Msaidizi Idara ya Biashara ya Kimataifa wa Kampuni Alec Lu.
Baadhi
wa watu mbalimbali walioshiriki ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa
zinazozalishwa nchini China yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya siku nne ambayo
yamefunguliwa leo yanalengo la kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini
humo ili viwanda na makampuni ya nchi hiyo yaweze kufanya biashara na
watanzania.Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments:
Post a Comment