Mkutano
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umemteua Said Hamad
El Maamry kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ambayo kazi yake kubwa
ni kusimamia mali za shirikisho.
El Maamry
ambaye kitaaluma ni mwanasheria na Mwenyekiti wa zamani wa TFF wakati
huo ikiwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania ataongoza bodi hiyo yenye
jumla ya wajumbe watano.
Wajumbe
wengine wa bodi hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ambaye
anakuwa Makamu Mwenyekiti, Dk. Ramadhan Dau, Mohamed Abdulaziz na
aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephen Mashishanga.
No comments:
Post a Comment