Uthibitisho huu umetoka kwa mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani
Tanzania (NECTA) Prof Rwekaza Mukandala kuwa Katibu Mtendaji wa NECTA Dr
Joyce Ndalichako ameondoka NECTA na nafasi yake sasa inakaimiwa na Dr
Charles Msonde aliyekuwa msaidizi wake.
Kwa mujibu wa Profesa Mukandala, ni kwamba Dr Ndalichako ameanza likizo
ya utafiti (Sabbatical leave) ya mwaka mmoja kuanzia Oktoba mosi mwaka
huu hadi Septemba 30 mwaka 2014 licha ya kuwepo kwa taarifa za kuwepo
shinikizo la kisiasa lilikuwa likimzonga Dr Ndalichako kutakiwa
kujiuzulu.Dr. Ndalichako
CHANZO: JAMII FORUM
|
No comments:
Post a Comment