Hatimaye Tumechagua Mabadiliko,
Salamu kwa wanafamilia wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Salamu kwa wapenda michezo wa ndani na nje ya nchi yetu Tanzania.
Naanza
kwa kumshukuru Mungu kwa hekima, busara, akili, vipaji na uwezo
aliotujaalia kutuwezesha kutenda yote haya kwa amani na utulivu.
Shukrani
za dhati zimwendee Bw. Leodegar Tenga, rais wa TFF 2005 - 2013
anayekabidhi madaraka kwa rais mpya wa TFF. Yeye na timu yake kwa hakika
wanastahili pongezi kwa mengi mazuri waliyofanya.
Shukrani
kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi 2013 kwa kunikubali, mimi Jamal
E. Malinzi niwe Rais wa TFF kwa kipindi kijacho cha miaka minne.
Kweli
dunia imekuwa kijiji, kwani kipindi cha masaa 72 baada ya kuzindua
ilani yangu ya uchaguzi, nimepokea salamu, maoni na mapendekezo toka
ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Burundi, Ivory Coast,
Denmark na NewZealand.
Kupitia www.jamalmalinzi.com, twitter @jamalmalinzi,
Jamii Forum, Facebook na mitandao mingine, naomba tuendelee
kuwasiliana, kutoa maoni, kukosoa na kuchangia mijadala yenye tija na
ufanisi ili Tanzania yote ipate neema ya mpira wa miguu.
Safari
ni ndefu na wasafiri ni wengi kwenye vyombo vichache vya usafiri. Kwa
wale ambao tayari wana ramani ya safari yetu, sote bila kujali tofauti
zetu hasa wakati wa kuwania uongozi, tutoe mchango wake ili Tanzania
isonge mbele katika ulimwengu wa soka.
Naam,
kuna msemo wa Kiswahili unaosema 'kukata tamaa ukingali unaishi ni
dhambi'. Naomba msemo huu na utuongoze kila tunapojikwaa tunanyuke na
kuendelea na safari hadi tufike tulipopakusudia.
Historia imeshaanza kuandikwa, mwaka 2013 ni Tumechagua Malinzi, Tumechagua Mabadiliko na sasa tunasonga mbele.
Jamal E. Malinzi
Oktoba 27, 2013
No comments:
Post a Comment