Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania -TRL umetangaza kusitishwa kwa huduma ya treni ya jiji hapo leo Jumatatu Oktoba 21, 2013 kufuatia ukarabati wa vichwa cha treni vinavyotoa huduma hiyo kutokamilika kwa wakati.katika karakana ya Morogoro.
Taarifa
za kiufundi zimebainisha kuwa ukarabati wa vichwa hivyo utakamilika
mapema leo asubuhi na hivyo kuwasili Dar jioni tayari kuanza huduma
keshokutwa Jumanne, Oktoba 22, 2013 kwa mujibu wa ratiba yake ya
kawaida..
Kuhusu
kichwa cha treni kilichopata hitilafu ya kuungua moto jana jioni kikiwa
safarini kutoka stesheni ya Kamata kuja kituo kikuu cha Dar ni
miongoni mwa ya vichwa vitatu vinavyofanyiwa ukarabati huko Morogoro.
Ukiwaomba
radhi Wakazi wa jiji ambao ni watumiaji wakubwa wa huduma hiyo
inayoanzia Stesheni ya Ubungo Maziwa hadi Stesheni ya Dar es salaam,
Uongozi umewahakikishia kuwa mafundi wa TRL katika karakana za Morogoro
na Dar es Salaam wanafanya kila jitihada kurejesha huduma hiyo kwa
wakati ili kupunguza usumbufu kwa wateja.wake ambao wameizoeya sana
huduma na kunufaika nayo.
Imetolewa kwa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaaam,
Oktoba 20, 2013
Midladjy Maez
No comments:
Post a Comment