Aomba msaada zaidi ili aanze tiba. Wataalamu wazungumzia ugonjwa wake, wasema unatibika.
Dar es Salaam. Katika toleo la ijumaa iliyopita tulizungumzia hali ya afya ya Seleman Rajab (17), mkazi wa Kivule, jijini Dar es Salaam.
Seleman licha ya kuwa anaumwa sana, mara ya mwisho kupelekwa hospitali ilikuwa mwaka 2010 kwa kuwa hana uwezo wa kufanya hivyo.
Hata hivyo, taarifa za awali za wataalamu wa afya
zinasema Seleman atakuwa anasumbuliwa na matende, ugonjwa ambao kwa umri
wake anaweza kutibiwa na kupona.
Seleman ana imani kuwa watu wakimsaidia vilivyo akapata nguvu kifedha, ataweza kupelekwa hospitali na hivyo kupona.
Awali Seleman alipoteza matumaini hasa kutokana na
ukweli kuwa licha ya kuwa na maumivu, amekuwa akiyatuliza kwa kumeza
dawa za kutuliza maumivu, kutokana na kutokuwa na uwezo wa kwenda
hospitali.
Baba Seleman anafanya kazi ya kutunza bustani
kwenye Kiwanda cha Kamal Steel, kinachotengeneza nondo, jijini Dar es
Salaam, mama yake ni mama wa nyumbani katika familia hiyo yenye watoto
watano, wa kike mmoja wa kiume. Wadogo zake wanasoma shule mbalimbali.
Baba Seleman anasema katika familia yao hakuwahi
kutokea mtu kuugua ugonjwa wa aina hiyo, ila baba mzazi wa mama yake
mguu wake mmoja una tende, umevimba sana lakini anasema yeye hutembea na
kufanya shughuli zake kama kawaida, tofauti na Seleman.
Sura ya Baba Seleman (Rajab) kwenye kidevu upande
wa kushoto ina uvimbe mkubwa kidogo, anasema umekuwapo kitambo sasa na
kwamba alienda Hospitali ya Amana akaandikiwa dawa za kutumia; “Hiki
kipo siku nyingi tu, wala hakiumi.”
Seleman alizaliwa akiwa na afya njema, lakini akiwa na uvimbe mdogo ambao uliendelea kukua kadri alivyokuwa anakua.
Ugonjwa wake
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya ugonjwa wa aina hiyo unaweza kuwa ni wa kurithi, lakini anaweza kupona akifanyiwa tiba sahihi.CHANZO GAZETI LA MWANANCHI
No comments:
Post a Comment