Usiku wa Alhamisi iliyopita, mkazi wa mtaa wa Malela, Mbagala, Jijini Dar es Salaam, Anna Mbago (35) aliuawa kwa kunyongwa na mtu aliyeingia chumbani kwake baada ya kutoboa dari.
Inaelezwa kuwa mtu huyo aliingia kupitia sebuleni,
Anna alisikia kishindo, alipotoka chumbani kwenda kuangalia ndipo
akakutana na muuaji ambaye alimnyonga.
Hata hivyo kabla ya umauti, Anna alipiga kelele
zilizosababisha baadhi ya majirani kuizingira nyumba. Kilio chake
hakikuzuia asiuawe kwa vile hata majirani walishindwa kuingia kwa vile
nyumba ilikuwa imefungwa; Muuaji aliendelea kumnyonga hadi kufa licha ya
kuomba asiuawe.
Majirani waliosikia kilio cha kuomba msaada
waliizingira nyumba hiyo wakihangaika namna ya kuingia ndani bila
mafanikio, kwani milango yote ilikuwa imefungwa.
Baadaye walitoa taarifa polisi kupitia kwa
Mwenyekiti wa Mtaa wa Malela, wakati askari wanafika Anna hakuwa
anaendelea kupiga kelele za kuomba msaada, huku wengi wakifikiri labda
amejificha au amekufa.
Polisi walipoingia walimkuta Anna kwenye korido,
akiwa hajitambui, walipompeleka hospitali ndipo ikathibitika kwamba
alikuwa amekufa.
Muuaji alikutwa amejificha chooni ndani ya nyumba
hiyo, anasema Mkuu wa Upelelezi katika Wilaya ya Kipolisi ya Mbagala,
Thobias Walelo.
Polisi wakiri kweli elimu haina mwisho
Wahenga walisema ‘Elimu haina mwisho’. Usemi huu
umethibitika kwa kamanda wa upelelezi wa Wilaya ya kipolisi Mbagala,
mkoani Temeke, Jijini Dar es Salaam, Thobias Walelo wakati akizungumzia
mauaji ya Anna Mbago (35).
“Unaposikiliza maelezo ya muuaji, ukizingatia
mazingira ya tukio, siyo rahisi kuamini kilichotokea, nakiri tukio hili
ni la aina yake kwangu, limenidhihirishia kuwa elimu haina mwisho,
napaswa kuendelea kujifunza zaidi kama ambavyo wanadamu tunapaswa
kuendelea kujifunza bila kuchoka hadi siku ya mwisho wa uhai
wetu,”anaeleza ASP Walelo.
Mtuhumiwa akijieleza;
“Naitwa (jina tunalo), ninafanya biashara ya sigara, naishi Mbagala” anasema mtuhumiwa wa mauaji hayo akiwa mikononi mwa polisi.CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment