Pages

Tuesday, October 1, 2013

Idadi ya waliopotea yapungua Kenya

kenya 2 f4ede
Shirika la msalaba mwekundu limesema kuwa idadi ya watu waliopotea kutokana na shambulizi la kigaidi la Westgate, imepungua hadi 39 kutoka 61, idadi iliyotangazwa awali na shirika hilo awali.

Kati ya watu hao, 14 wamepatikana wakiwa hai na miili saba ikipatikana katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Kwa mujibu wa serikali, watu 67 waliuawa baada ya wanamgambo wa Al Shabaab kuvamia jengo la Westgate mjini Nairobi, tarehe 21 Septemba.
Wabunge wameanza kuchunguza taarifa za ulegevu upande wa maafisa wa ujasusi na wa serikali.
Shirika la Red Cross linasema kuwa baadhi ya jamaa za wale waliokuwa wameripotiwa kupotea kwa jamaa zao, hawakutoa taarifa wakati walipowapata.
Afisaa mmoja wa shirika hilo, ameambia BBC kuwa baadhi ya ripoti walizokuwa nazo zilikuwa kutoka kwa jamaa waliokuwa na wakati mgumu kuwapata watu wao.
Serikali ilisema kuwa hadi sasa hakuna watu wowote ambao wanasemekana kupotea baada ya kutokea shambulizi hilo na kuwa hakuna mateka wowote waliouawa wakati jengo la Westgate lilipoporomoka.
Hata hivyo, vifusi vingali vinaondolewa na kwa hilo waziri wa usalama akasema kuwa miili zaidi huenda ikapatikana.
Magaidi watano waliuawa na vikosi vya usalama, wakati wa uvamizi huo wakati watu tisa wakikamatwa kuhusiana na shambulizi hilo la kigaidi.
Kundi la kigaidi la Al Shabaab lilikiri kutekeleza mashambulizi hayo kulipiza kisasi hatua ya Kenya kujihusisha na vita nchini Somalia. Chanzo: bbcswahili

No comments:

Post a Comment