Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Advocatus Kakorozya akimwelezea jinsi
tasisi inavyotumia teknologia kupata taarifa mbalimbali za afya ambazo
zimesaidia sana serikali kutunga sera.
Rais
Jakaya Kikwete alitembelea kituo cha Bagamoyo ya Taasisi ya Afya ya
Ifakara (IHI) na kuonyeshwa kazi mbalimbali za utafiti zinazofanyika
kituoni hapo. Raisi Kikwete aliisifia taasisi hiyo kwa kufanya kazi
kubwa hasa katika upande wa ugonjwa wa Malaria na kujipatia sifa kubwa
duniani.
Rais
Kikwete akimsikiliza mtafiti wa IHI Dk Nico Govella akimpa maelezo juu
ya utafiti wake ambapo magunia ya katani yakichanganywa na kemikali
fulani yanaweza kutumika kukinga wanadamu dhidi ya mbu wanaoeneza
malaria.
Rais Kikwete akimsikiliza Grace Mwangoka wa IHI akimweleza shughuli mbalimbali za maabara kwenye taasisi hiyo.
Rais
Kikwete akimsikiliza Joseph Madata ambaye ni mkutubi akimwelezea
matumizi ya maktaba mtandao (digital library) ya taasisi hiyo.
Rais
Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa IHI pamoja na
wenzao kutoka Equatorial Guinea ambao wapo kwenye kituo hicho cha
Bagamoyo kwa ajili ya mafunzo.
No comments:
Post a Comment