Mkuu wa mkoa wa Njombe Kepten Mstaafu Asser Msangi akitoa taarifa ya uzinduzi wa mkoa wa Njombe leo katika ukumbi wa RC
Na Francis Godwin Blog Njombe
Serikali
mkoa wa Njombe imetangaza ratiba kamili ya uzinduzi wa mkoa mpya wa
Njombe ambapo mkoa huo sasa utazinduliwa rasmi na Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete Octoba 16 mwaka huu.
Mkuu wa
mkoa wa Njombe Kepten Mstaafu Asser Msangi ametoa taarifa hiyo leo
katika ukumbi wa RC mjini Makambako kuwa siku ya tarehe 16 mara baada ya
Rais Kikwete kutoka mkoa wa Iringa katika kilele cha mbio za mwenge wa
Uhuru kitakachomalizika kitaifa mkoani Iringa atafanya uzunduzi wa mkoa
huo wa Njombe katika uwanja wa saba saba pamoja na kuweka jiwe la msingi
katika ofisi ya Halmashauri ya mji wa Njombe.
Hata
hivyo alisema siku inayofuata ambayo ni Octoba 17 mheshimiwa Rais
Kikwete atakuwa wilaya ya Makete ambapo shughuli atakazozifanya ni
pamoja na kusalimia wananchi wa kijiji cha Kipengere ,kuweka jiwe la
msingi sekondari ya Lupalilo,kuweka jiwe la msingi Zahanati ya
Ivalalila,kuzindua chuo cha VETA na baadae kuwahotubia wananchi katika
mkutano utakaofanyika uwanja wa Iwawa mjini Makete .
Mkuu huyo
wa mkoa alisema kuwa Octioba 18 Rais Kikwete atafanya ziara katika eneo
la Lupembe Njombe kwa kuzindua kiwanda kipya cha Chai Cha Iganga Tea
Company ,kuweka jiwe la msingi mradi wa umeme wa Mapembasi uliopo
Halmashauri ya mji .
Wakati
Octoba 19 atakuwa wilaya ya Ludewa ambako atazindua maabara ya kisasa
katika Hospital ya wilaya ya Ludewa na baada ya hapo atafanya mkutano wa
hadhara katika uwanja wa Ludewa mjini .
Katika
ziara hiyo wilayani Ludewa Octoba 20 atatembelea mradi wa Liganga(Chuma)
katika kijiji cha Mndindi kabla ya kuondoka kuelekea mjini Njombe kwa
mapumziko huku Octoba 21 Rais Kikwete atafanya majumuisho ya ziara yake
mkoa mpya wa Njombe katika ukumbi wa Halmashauri ya Njombe kabla ya
kuondoka mkoani hapo.
Hivyo
amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa mkoa huo
pamoja na maeneo ya miradi ambayo Rais Kikwete atapita mkoani humo.
No comments:
Post a Comment