TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Alhamisi Oktoba 3, 2013
Ziara ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Uingereza na Mkuu wa Diplomasia katika ofisi ya mambo ya nje na Jumuiya ya Madola
Ziara
hii inatoa taswira ya umuhimu wa kihistoria na kimkakati unaoendelea
baina ya Tanzania na Uingereza na kudhihirisha mahusiano bora yaliyopo.
Uingereza tayari ni mwekezaji mkubwa nchini Tanzania na ni mfadhili
mkubwa wa pili. Kwa mwaka
huu
pekee, Idara ya Maendeleon ya Kimataifa ya Uingereza yenye kuratibu
shughuli za maendeleeo (DFID) itatumia Paundi Milioni 150 (sawa na TZS
390 Bilioni) katika shughuli za maendeleo nchini Tanzania.
Ziara
ya Sir Simon inafuatia mafanikio makubwa ya ziara ya Waziri wa
Uingereza mwenye dhamana ya Afrika, Mark Simmonds, mwezi Julai ambapo
Rais Kikwete aliafiki mahusiano mapya ya juu kati ya Uingereza na
Tanzania katika kusimamia ustawi, mahusiano ambayo yanaongozwa na Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda yanayotoa fursa zenye kusisimua katika maeneo ya
uziduaji (extractive industry), kilimo na sekta ya nishati endelevu
vilevile mazingira ya kibiashara kwa upana wake. Matumaini ya Uingereza
kupitia ushirikiano wa kibiashara ni kuongeza biashara na uwekezaji na
kusaidia maendeleo ya Tanzania na kuzaa ustawi na ajira kwa Tanzania na
Uingereza. Hii inaenda sambamba na msaada wa Uingereza kwa serikali ya
Tanzania katika mpango wa Matokeo Makubwa Sasa.
Akizungumza kabla ya ziara, Sir Simon alisema:
“Uingereza
inaiona Tanzania kama moja ya wadau wake muhimu sana Afrika na ninayo
fahari kuitembelea kwa mara ya kwanza. Ninatarajia kusikia mwenyewe toka
kwa wahusika wenyewe juu ya uwepo wa fursa nyingi nchini Tanzania na
kuelewa vyema namna gani Uingereza inaweza kuiongeza tija.
Licha
ya kwamba Uingereza tayari inaongoza katika uwekezaji Tanzania, bado
tunahitaji kuwekeza zaidi. Tunataka kufanya kazi kwa ushirika kusaidia
Tanzania kuweza kufikia malengo ya kuwa taifa la uchumi wa kati ifikapo
mwaka 2025 na kunufaisha wananchi wake wote. Tunataka kufanya haya kwa
dhamira ya kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi zetu mbili na
kuendelea kuisaidia Tanzania kimaendeleo. Ni matumaini yangu katika
zaira yangu italeta matunda katika ushirikiano wetu wa kiuchumi na
kutafuta namna ya kusaidia kuboresha mazingira ya kibiashara”
Katika
ziara yake, Sir Simon atakutana na Waziri wa Viwanda na Biashara, na
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji na
Uwezeshaji, Viongozi toka Kitengo cha Rais-Utekelezaji (President’s
Delivery Bureau), na makampuni kadhaa ya Uingereza, Mfuko wa Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania.
__________________________________________________________
Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na;
Michael Dalali
Afisa Miradi na Habari
Ubalozi wa Uingereza
Dar es Salaam
Simu: +255 (0) 22 229 0269
Simu ya Mkononi: +255 (0)762 791 991
Baruapepe: michael.dalali@fco.gov.uk
No comments:
Post a Comment