Na Boniface Wambura, TFF
Kiingilio
cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na
Yanga itakayochezwa Jumapili (Octoba 20 mwaka huu) kitakuwa sh. 5,000.
Kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.
Kwa
upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi
ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B
itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja
itapatikana kwa sh. 30,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni katika vituo mbalimbali.
Vituo
hivyo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa
Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta
Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza
Madukani.
Mechi
hiyo namba 63 itachezeshwa na Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam,
ambapo atasaidiwa na Hamis Changwalu wa Dar es Salaam pia, na Ferdinand
Chacha wa Bukoba. Mwamuzi wa akiba ni Oden Mbaga wa Dar es Salaam.
Kamishna
wa mechi hiyo atakuwa John Kiteve kutoka Iringa wakati mtathmini wa
waamuzi (referees assessor) ni Stanley Lugenge wa Njombe.
MECHI TATU FDL ZASOGEZWA MBELE
Mechi
tatu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) katika kundi A na C zimesogezwa
mbele kutokana na viwanja vya Kambarage, Shinyanga na Nangwanda Sijaona,
Mtwara kuwa na shughuli nyingine za kijamii.
Katika
kundi A, mechi kati ya Ndanda na Transit Camp iliyokuwa ichezwe Oktoba
19 mwaka huu sasa itafanyika Oktoba 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Nangwanda Sijaona.
Stand
United na JKT Kanembwa zilizokuwa zicheze Oktoba 19 mwaka huu, sasa
mechi hiyo ya kundi C itafanyika Novemba 2 mwaka huu Uwanja wa Kambarage
mjini Shinyanga. Nayo mechi ya Mwadui na Polisi Dodoma iliyokuwa
ichezwe kwenye uwanja huo Oktoba 26 mwaka huu imesogezwa hadi Novemba 3
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment