Matukio
yenyewe yanakuwaje: Watu hao hutangaza nafasi za kazi mbali mbali
kupitia mitandao hiyo kwa kuandika wana makampuni na wanatafuta watu kwa
nafasi mbambali kwenye makampuni yao feki, kwa kutambua watanzania
wengi wana shida ya ajira hutangaza nafasi ambazo wanaamini wengi
wataziomba na kuweka vigezo vya chini sana hasa eneo la Elimu na
uzoefu kwa kuamini wengi wataomba, baada ya hapo, wewe mwenye shida ya
ajira ukishatuma CV yako ambayo itakuwa pia inaonyesha mawasiliano yako,
wao hutumia mwanya huo kukutumia ujumbe mfupi (SMS) na kujifanya wao ni
wafanyakazi wa kampuni husika ambayo imetangaza nafasi hiyo na kujidai
wanaweza kukusaidia kuipata kazi hiyo na kukutaka uwatumie hela ili
wakufanyie mpango na kukutumia maswali ambayo utaulizwa kwenye INTERVIEW
na majibu yake, hawa jamaa kwa kutambua shida ya Watanzania hawasemi
wanataka kiasi kikubwa huwa wanataka kiasi cha Elfu kumi hadi Hamsini,
wanafanya hivyo kwa kutambua wewe mtafuta ajira unaweza ukakipata kiasi
hicho.
Matapeli
hao hudiriki kukwambia na kiasi cha mshahara ambao utalipwa kwenye kazi
hiyo ili kukutamanisha utume hiyo hela, simu hiyo ambayo imekutumia
ujumbe huo ukiipigia huwa haipatikani na ikipatikana haipokelewi na
wanakua wameziregister kwa majina ambayo wanakuaminisha ni yao kumbe ni
majina ya uongo ya kutapelia watu.
Mpaka
sasa wameshawaliza watu wengi sana kwa hiyo wewe mdau kuwa makini sana
wakati unaomba ajira kupitia mitandao mbalimbali ya Internet, ukiona
unaombwa hela baada ya kuomba ajira kupitia mitandao hiyo ujue ndio hao
matapeli.
KUWA MAKINI EWE MTANZANIA
IMETOLEWA NA:
MDAU MPENDA HAKI
No comments:
Post a Comment