JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
IDARA YA UHAMIAJI
TAARIFA
KWA UMMA
YAH:
MABADILIKO YA MAAFISA UHAMIAJI WA MIKOA,
WILAYA NA VITUO.
Kamishna Mkuu wa
Uhamiaji, Sylvester Ambokile, amefanya mabadiliko katika safu ya Maafisa
Uhamiaji wa Mikoa, Wilaya na Wafawidhi wa Vituo mbalimbali nchini
Katika mabadiliko
hayo Kamishna Mkuu Ambokile amewateua, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Jacob Sambai
aliyekuwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Manyara kuwa Msaidizi wa Afisa Uhamiaji Mkoa
wa Mtwara na nafasi yake inachukuliwa na Naibu Kamishna Barikieli Shayo kutoka
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati Naibu Kamishna wa Uhamiaji Augustino
Haule ametuliwa kuwa Afisa Uhamiaji wa Mkoa Morogoro.
Mabadiliko pia
yamefanyika kwa Vitengo vya Makao Makuu,Wafawidhi wa Vituo pamoja na Maafisa
Uhamiaji wa Wilaya. Katika mabadiliko hayo Naibu Kamishna Hilgaty Shauri
aliyekuwa Mdhibiti wa Pasipoti Makao Makuu anakuwa Afisa Uhamiaji Wilaya ya
Kinondoni na nafasi yake kuchukuliwa na
Naibu Kamishna Abuu Mvano ambae kabla ya mabadiliko hayo alikuwa ni Mfawidhi
wa kituo cha Uhamiaji katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), wakati
Naibu Kamishna Safina Muhindi ameteuliwa kuwa Afisa Uhamiaji wa Wilaya
Kinondoni. Wengine ni Naibu Kamishna Fredrick Kiondo aliyekuwa Mfawidhi Kituo
cha Holili anayekuwa Mfawadhi KIA, wakati
nafasi yake inachukuliwa Naibu Kamishna
Estomih Urio ambae kabla ya uteuzi huu
alikuwa ni Afisa Uhamiaji Wilaya ya Karatu. Naibu Kamishna Apolinary Msuya
ameteuliwa kuwa Afisa Uhamiaji Wilaya ya Karatu akitokea Ofisi ya Uhamiaji Tarakea Mkoani Kilimanjaro. Naibu Kamishna
Evarist Mlay kutoka Tunduma anahamia
Mkoa wa Dar es Salaam na nafasi yake inachukuliwa Naibu Kamishna Alphonce
Kwikubya aliyekuwa Afisa Uhamiaji Wilaya ya Kinondoni akisaidiwa na Naibu
Kamishna Lusarago Mreka kutoka Makao Makuu.
Naibu Kamishna
Sipora Moshi aliyekuwa Mfawidhi Kituo cha Bandari ya Dar es Salam ameteuliwa
kuwa Mkuu wa Kitengo cha Ubalozi Makao Makuu ya Uhamiaji na nafasi yake
inachukuliwa na Naibu Kamishna Harride Mwaipyana aliyekuwa Ofisi ya Uhamiaji
Kabanga. Wakati huo huo
Mabadiliko hayo ambayo
yanaanza mara moja ni sehemu ya kuimarisha utendaji kazi na uwajibikaji ndani
ya Idara ya uhamiaji katika kuwahudumia wananchi, kuwezesha uingiaji na utokaji
wa watu pamoja na udhibiti wa wageni nchini. Akizungumzia mabadiliko hayo,
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abbas Irovya,
alieleza kwamba Idara imeandaa mkakati wa maboresho ya kitaasisi, rasilimali
watu pamoja na vitendea kazi ili kuhakikisha kwamba watumishi wanaondokana na
utendaji wa mazoea.
“Katika
kulifanikisha hilo,” anasema Naibu Kamishna Irovya, “Idara ya uhamiaji imeandaa
Mkataba wa Huduma kwa Mteja ambao utazinduliwa hivi karibuni kwa nia ya
kuhakikisha kwamba huduma zinatolewa kwa wakati na kwa kuzingatia viwango
vinavyotakiwa. Mkataba huo utawapatia pia wadau wa huduma za uhamiaji fursa ya
kufahamu haki zao, wajibu walionao katika kupata haki hizo na mfumo mzima wakutoa
mrejesho kuhusu kuduma wanazopata’’.
Mabadiliko hayo yanakuja
katika kipindi cha mwezi mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
amteue Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Sylverster Ambokile kuongoza Idara ya
Uhamiaji, akichukua nafasi ya Magnus Ulungi ambaye amepangiwa majukumu mengine.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA
UHUSIANO
MAKAO MAKUU YA IDARA IDARA YA
UHAMIAJI.
No comments:
Post a Comment