CHADEMA NA CCM WAKICHAPANA. PICHA NA MAKTABA |
Tukio hilo la aina yake lilitokea majira ya saa 11 jioni katika ukumbi namba 40 uliopo kwenye jengo la Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Mapema Nanyaro aliwasilisha hoja kuhusu
ukusanyaji wa ushuru katika Soko la Kilombero, akidai kuwapo kwa
ubadhirifu wa ukusanyaji unaosimamiwa na baadhi ya watendaji wa Wilaya
ya Arusha akimhusisha pia Mkuu wa Wilaya hiyo, John Mongella.
Lakini kwa upande wake, Diwani wa Kata ya
Terati, Julius Ole Sekeyani, alimpinga diwani mwenzake akitaka Mkuu wa
Wilaya asishambuliwe kwa kuwa hahusiki na ukusanyaji wa ushuru sokoni
hapo na wala hajawahi kufanya hivyo, madai ambayo yalisikika kupingwa na
madiwani wengine.
Akitoa ufafanuzi kuhusu hilo, Mweka Hazina
wa Jiji, Kessy Mpakata, alisema mkuu wa soko asubuhi anatoa vitabu vya
kukusanyia ushuru kwa vijana maalum walioajiriwa kwa kazi hiyo ambao
huvirudishwa tena kwake baada ya soko kufungwa majira ya jioni.
Alisema mkuu wa wilaya hahusiki kabisa na utaratibu huo.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida iliyodumu
kwa dakika chache, wakati maelezo na ufafanuzi huo ukitolewa, Doita na
Nanyaro walipandisha jazba na kutaka kumvaa diwani Ole Sekeyani.
Nanyaro alimtaka Ole Sekeyani kuzungumza kwa lugha ya kawaida na siyo ya kejeli na dharau.
Purukushani hizo zilimfanya mwenyekiti wa
kikoa hicho, Diwani wa Kata ya Daraja Mbili, Prosper Msofe (Chadema),
kuahirisha kikao hicho majira ya saa 12 jioni hadi tarehe nyingine
itakayotangazwa.
Mapema Baraza hilo lilitoa muda wa miezi
minne kwa watendaji wa Idara ya Ardhi kuhakikisha wanaweka mipaka maeneo
ya vyanzo vya maji, milima na barabara kwa lengo la kuzuia ujenzi
holela.
CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment