Nchini Burundi, Bwana Bernard
Busokoza wa kabila wa watutsi na anayetoka chama cha Uprona, ameteuliwa
kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Burundi .
Bernard Busokoza mwenye umri wa miaka 60 ,
anachukua nafasi ya Terence Sinunguruza aliyejiuzulu hivi karibuni baada
ya kupoteza imani ya chama chake cha Uprona kwa madai kwamba alipuuza
maslahi ya chama na kujiendeleza yeye binafsi.Anamiliki mojawapo ya kampuni kubwa ya mawasiliano nchini humo.
Uteuzi huo wa Bernard Busokoza umeidhinishwa Jumatanojioni na bunge pamoja na baraza la seneti.
Hata hivyo kulikuwa na pingamizi kuhusu uteuzi wake hasa kutoka kwa wabunge wa chama cha (CNDDFDD) cha Rais Pierre Nkurunzinza wakisema kuwa aliwahi kuhusika na mapinduzi ya kijeshi yaliyosababisha kifo cha rais wa kwanza wa kihutu Milkior Ndadai
Makamu wa rais aliyemtangulia, Terence Sinunguruza alijiuzulu kutokana na shinikizo za wanachama wenzake wa (UPRONA) waliodai kuwa haonekani kutetea masilahi ya chama chake.
Chama hicho kilimtaka Rais Pierre Nkurunziza kumfuta kazi Sinunguruza, aliyetuhumiwa kwa kusababisha migawanyiko chamani tangu kuchukua wadhifa huo miaka mitatu iliyopita.
No comments:
Post a Comment