Pages

Wednesday, October 2, 2013

MBOWE AKATIZA ZIARA YAKE NCHINI DENMARK ili KUSHIRIKI MSIBA WA DADA YAKE


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ameamua kukakatiza ziara yake nchini Denmark ili kushiriki msiba wa dada yake mpendwa aitwaye Grace Mbowe aliyefariki dunia juzi (Jumapili). Marehemu Grace alifariki kwa ajali ya gari katika kata ya Kabuku wilayani Handeni, mkoani Tanga. Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amen!

No comments:

Post a Comment