Pages

Tuesday, October 15, 2013

Mchezaji wa Nigeria ajeruhiwa Ethiopia

131014172849_nigeria_player_304x171_bbc_nocredit_b112b.jpg
Mchezaji soka wa Nigeria, Nosa Igiebor alijeruhiwa vibaya wakati timu yao iliposhambuliwa mjini Addis Ababa baada ya mchuano wao wa mchujo dhidi ya Ethiopia katika kutafuta nafasi ya kushirki kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil.
Mchezaji huyo ambaye huchezea timu ya Real Betis alihitaji matibabu ya dharura mkononi mwake baada ya dirisha la basi walimokuwa kuvunjwa wakati timu hiyo ilipokua inaondoka kutika mji mkuu Addis Ababa.Alijeruhiwa kwa vigae vya glasi.
Nigeria, ilishinda mabao mawili kwa moja na wameripoti tukio hilo kwa Fifa.
"Tunatumai kuwa Fifa itachukua hatua za kinidhamu," alisema makamu rais wa shirikisho la soka la Nigeria Mike Umeh.(P.T)
"Ni jambo la aibu sana kwa tukio kama hili lilitokea baada ya mechi."
Ben Alaiya, afisaa wa uhusiano mwema wa timu ya taifa ya Super Eagles alimuunga mkono Umeh katika kulaani tukio hilo.
Alaiya alisema kuwa mashabiki walishambulia basi iliyokuwa imewabeba wachezaji wa timu ya Nigeria kwa mawe ambayo yalivunja mojawapo ya dirisha la basi hivyo kulazimisha wachezaji kukimbilia usalama wao
Waliseama kuwa Igiebor hakubahatika kwani jiwe liligonga mkono wake na kusababisha damu kuvuja sana
Super Eagles wa Nigeria ndio wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kufuzu kucheza katika michuano ya kuwania kombe la dunia watakapocheza mechi ya marudiano mjini Calabar tarehe 16 Novemba.

No comments:

Post a Comment