Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, October 2, 2013

Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF waanza rasmi leo jijini Arusha


Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Oktoba 2 mpaka Oktoba 5,2013.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF,Dk. Aggrey  Mlimuka akitoa hotuba yake mapema leo asubuhi wakati wa ufunguzi  wa Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa  PPF unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini  Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio akizungumza leo kwenye  Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,unaofanyika leo  kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Lulu Mengele akifafanua jambo juu  ya Muonekano wa Logo Mpya ya Mfuko huo iliyozinduliwa Rasmi leo kwenye  Ukumbu wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Chama cha Wakuu wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii nchini,Daudi Msangi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi na kwa wadau wote kwa ujumla kwa  kuitika kwao wito kwenye Mkutano huo.
Bw. Bonda Nkinga akitoa Ushuhuda wake wake mbele ya  Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa  Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kuwasaidia watoto zake kusoma kupitia Fao la elimu.
Kijana Peter William Mulokozi ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari ya Mzumbe akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Baba yake kupoteza maisha ghafla.PPF ambao ni Mfuko pekee unaotoa fao la Elimu nchini endapo Mwanachama anakuwa amefariki akiwa kwenye ajira.PPF imeweza kumsaidia kijana huyu kusoma mpaka hapo alipofikia.
Kijana Pascalia Nsatto ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Kimataifa ya Moshi akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Wazazi wake wote wawili kupoteza maisha.
Ilikuwa ni huzuni tu wakati vijana hao wakitoa ushuhuda wao wa namna walivyoweza kusaidiwa kimasomo na Mfuko wa Pensheni wa PPF pindi walipoondokewa na wazazi wao.

No comments:

Post a Comment