Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 23
wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa
Fedha,Dkt William Mgimwa akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo
unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini
Arusha kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Oktoba 2 mpaka Oktoba 5,2013.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF,Dk. Aggrey Mlimuka akitoa hotuba
yake mapema leo asubuhi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Mwaka wa
Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika kwenye
ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF,William Erio akizungumza leo kwenye Mkutano wa 23 wa
Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,unaofanyika leo kwenye ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF,Lulu Mengele akifafanua jambo juu ya Muonekano wa Logo
Mpya ya Mfuko huo iliyozinduliwa Rasmi leo kwenye Ukumbu wa Kimataifa
wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Chama cha Wakuu wa
Mashirika ya Hifadhi za Jamii nchini,Daudi Msangi akitoa shukrani kwa
mgeni rasmi na kwa wadau wote kwa ujumla kwa kuitika kwao wito kwenye
Mkutano huo.
Bw. Bonda Nkinga akitoa Ushuhuda
wake wake mbele ya Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye
Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kuwasaidia watoto zake
kusoma kupitia Fao la elimu.
Kijana Peter William Mulokozi
ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari ya
Mzumbe akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana na Wadau wa PPF
waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza
kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Baba yake kupoteza maisha ghafla.PPF
ambao ni Mfuko pekee unaotoa fao la Elimu nchini endapo Mwanachama
anakuwa amefariki akiwa kwenye ajira.PPF imeweza kumsaidia kijana huyu
kusoma mpaka hapo alipofikia.
Kijana Pascalia Nsatto ambaye ni
Mwanafunzi wa Kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Kimataifa ya
Moshi akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana na Wadau wa PPF
waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza
kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Wazazi wake wote wawili kupoteza
maisha.
Ilikuwa ni huzuni tu wakati vijana
hao wakitoa ushuhuda wao wa namna walivyoweza kusaidiwa kimasomo na
Mfuko wa Pensheni wa PPF pindi walipoondokewa na wazazi wao.
No comments:
Post a Comment