Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, October 14, 2013

MKUTANO WA KWANZA NA VIJANA WA BAJAJI NA BODABODA WA MKOA MZIMA WA DAR ES SALAAM

TAREHE NA MDA : (Mkutano huu wa kwanza utafanyika tarehe 14/10/2013 saa tatu kamili aubuhi (9:00AM) katika ukumbi wa HEKO HALL SINZA KARIBU NA KITUO CHA BAJAJI CHA AFRIKA SANA)

WASHIRIKI: Zaidi ya waendesha Boda boda 200 watahudhuia.

Asasi ya ya kitaifa ya afya ya umma (UHAI Tanzania) United Health Action Initiatives-UHAI imeandaa mkutano wa kwanza na vijana wa Bajaji na Bodaboda kwa mkoa mzima wa Dar es Salaam kuwapa elimu na maarifa yakuanzisha Benki ya Vijana iitwayo Ajira Vijana Foundation Bank -AVFB. Lengo ni kuwakuza nakuwatoa sekta isiyo rasmi kwenda sekta iliyo rasmi ya biashara.

Ili kufanikisha kwa haraka programu au mpango wa matokeo makubwa yakibiashara yani (BIG BUSINESS RESULTS NOW).

Benki hii itaanzishwa na vijana wa aina zote. Yaani;

Boda boda
Bajaji
Wanafunzi wa vyuo
Wanafunzi shule za msingi
Wanafunzi shule za sekondari
wamachinga
Wanaofanya kazi baa
Wanaofanya kazi hotelini
Mateja
Wanaofanya kazi guest house
Vijana wakulima vijijini

Na watu wengine katika jamii wenye umri zaidi ya umri wa ujana LAKINI WENYE KUBADILIKA NA KUWA NA MTAZAMO WA UJANA.

Lengo kuu ni kumfanya kijana kuchangia fedha kuanzia shilingi hamsini (Tsh. 50) ili waimiliki kabisa kabisa

Malengo madogoni;

Kukopa katika benki hii bila kuweka dhamana yoyoye ile

Kutumia umoja na mshikamano wao kama wakazi/eneo husika

kutambuana na kuomba mikopo

Kuwafanya vijana waliokubali kuchangia kuanzishwa kwa benki hii kuwa ndio wafanyakazi wa kazi zozote ndani ya benki na kwenye jamii

Kutoa riba ya chini zaidi kabisa ili kumsaidia mwanachama na jamii yake

Kutoa misaada yakuinua ubora wa elimu kwa maana ya SEMA na afya kwa maana ya MMAM na biashara kupitia Big Business Results Now (BRN).

WOTE MNAKARIBISHWA SANA. Imetolewa na Asasi ya UHAI.TANZANIA>>>http://uhai.or.tz/.

CONTACT THE UHAI MD DEUS NSHEKANABO ON 0714 418 190, 0763 772 88, 0773 025 698

No comments:

Post a Comment