By LASTECK ALFRED
In Summary
Mshahara wa Sh 200,000 ambao analipwa mchezaji wa
juu wa Ashanti ni sawa ya bei ya kiatu ambacho anavaa uwanjani Ngassa,
Kavumbagu, Niyonzima, Amis Tambwe au John Bocco.
WAKATI watu kama, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngassa, Didier Kavumbagu, Amis Tambwe, Abel Dhaira na Kipre Tchetche wanalipwa mishahara ya zaidi ya Sh 2 milioni kwa mwezi kila mmoja, mchezaji ghali wa Ashanti United analipwa Sh.200,000.
Hiyo ina maana kwamba mshahara wa Niyonzima pekee
yake, unaweza kulipa wachezaji 11 wa kikosi cha kwanza cha Ashanti
United ambacho kinaanza mechi yoyote.
Mshahara wa Sh 200,000 ambao analipwa mchezaji wa
juu wa Ashanti ni sawa ya bei ya kiatu ambacho anavaa uwanjani Ngassa,
Kavumbagu, Niyonzima, Amis Tambwe au John Bocco.
Si hilo tu, Ashanti inatumia Sh 8.5 milioni kulipa mishahara ya wachezaji na viongozi kila mwezi.
Katibu wa Ashanti United, Aboubakary Silas
alilifahamisha Mwanaspoti kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi
anapata Sh. 200,000 za Kitanzania na posho ya Sh.5,000 kila siku mara
baada ya mazoezi.
“Hatuna fedha za kulipa mishahara mikubwa,
tunajitahidi angalau kuwapa posho kila baada ya mazoezi pamoja na
kuwagharimia huduma za afya, maji na hata kulipia kambi siku moja au
mbili kabla ya kucheza mechi,” alisema Silas na kufafanua kuwa wana
wachezaji sita wanaosoma elimu ya juu kwa sasa kwenye kikosi hicho.
Wachezaji hao ni Roland Nasis, Ibrahim Himid,
Shabani, Wambong Mkongo (wote Chuo cha Elimu ya Biashara ‘CBE’), Imam
Ali (Chuo cha Usimamizi wa Fedha ‘IFM’) na Hussein Mohamed (anayesoma
Chuo cha Uhasibu Dar es Salaam ‘DSA’).
“Unapokuwa na wachezaji wasomi inasaidia wachezaji
wengine kujua ni mambo gani mazuri na yapi mabaya kwa kuwa mfano mzuri
kwa wenzao.”
Naye mchezaji wa zamani wa Simba Boniface Pawasa
ambaye ana elimu ya diploma ya masoko alisema: “Bila elimu maisha yangu
yangekuwa magumu hasa baada ya soka. Niliamua kurudi darasani ili
niishi vizuri kwenye dunia ya sasa yenye kuendeshwa na wasomi.”
Pawasa pia alizitaka timu kubadili programu zao
ili kutoa fursa kwa wachezaji kusoma na kujiendeleza kwenye mambo yao
binafsi huku akiwasisitizia wachezaji nao kutambua kuwa soka lina
mwisho.
No comments:
Post a Comment