Naibu
waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, Mhe. Januari Makamba
(kushoto) akiteta jambo na meya wa manispaa ya kinondoni, Yusuph Mwenda.Naibu
waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, Mhe. Januari Makamba
(kushoto) akizungumza na wakazi wa manispaa ya kionondoni. kushoto kwake
ni meya wa manispaa hiyo Yusuph Mwenda na naibu meya wa manispaa hiyo
Songoro Mnyonge.Mshambuliaji wa Mwananyamala Rashidi Kidebe (kushoto0 akiwania mpira na beki wa kawe kombaini Emmanuel Nengu.Naibu
waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, Januari Makamba (kushoto)
akikabidhi jezi kwa nahodha wa timu ya kawe Issa Kitasa ambao ni
washindi wa pili wa michuano hiyo.Naibu
waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, Januari Makamba
(katikati) akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya kawe Issa Kitasa
ambao ni washindi wa pili wa michuano hiyo. kulia ni meya wa manispaa
hiyo, yusuph mwenda.Naibu
waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, Januari Makamba (wa pili
kulia) akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya Mwananyamala, Ramadhani
kipanya baada ya timu yake kuibuka mabingwa wa michuano ya kombe la meya
wa kinondoni. kulia ni meya wa manispaa hiyo, yusuf mwenda.
Na Fadhili Akida
Mwananyamala
mabingwa wa kombe la meya wa kionondoni dhidi ya kawe kombaini,
wakabidhiwa bajaji, fedha tasilimu milioni 2 na jezi katika fainali
iliyofanyika uwanja wa magunia, msasani dar es salaam.
Timu
ya soka ya Mwananyamala jana waliibuka mabingwa wa kombe la meya wa
kinondoni na kukabidhiwa zawadi za bajaji, fedha tasilimu milioni 2 na
jezi. akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo naibu waziri wa
mawasiliano, sayansi na teknolojia, januari makamba aliwaasa vijana hao
kutumia vema zawadi hizo ikiwemo fedha na bajaj kwa kusaidia maendeleo
yao ikiwemo kuboresha maisha yao. makamba alimsifu meya wa manispaa hiyo
yusuph mwenda kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yanasaidia kuwaleta
vijana pamoja na kudumisha mshikamano na amani baina yao. kwa upande
wake meya wa manispaa hiyo, yusuf mwenda alisema huo ni mwanzo tu wa
kampeni yake ya kuweka safi manispaa yake ambapo kupitia michezo
anawahamasisha wakazi wa manispaa hiyo kuweka safi mazingira
yanayowazunguka.
No comments:
Post a Comment