Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipokea bendera
ya Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano
ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) kutoka kwa mwenyekiti wa
baraza hilo anayemaliza muda wake ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini
Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana. Dk Nchimbi sasa ni Mwenyekiti mpya wa RECSA
ambaye anaiongoza kwa kipindi cha miaka miwili. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Nchi wanachama
wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na
Tanzania. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment