Pages

Saturday, October 5, 2013

PICHA::KWA MARA YA KWANZA WANAINCHI WACHACHE WAJITOKEZA KUMSIKILIZA MBUNGE WA IRINGA MSIGWA

 



a_ac5ee.jpg
mwakilishi kutoka shirika la hifadhi la nyanda za juu kusini Godwell ole meing'ataki wa pili kushoto akiwa na waziri kivuli wa maliasili na utalii mbunge Peter Msigwa ambae alikuwa mgeni rasimi leo katika maadhimisho ya Tembo Duniani
b_9cf2c.jpg
c_567e5.jpg
Hawa ndio waliofika kumsikiliza mbunge Msigwa leo uwanja wa historia wa Mwembetogwa ambao kawaida huwa anajaza umati wa watu ila leo patupu

d_93871.jpg

Wananchi wa jimbo la Iringa mjini wakimsikiliza mbunge Msigwae_c624a.jpg
Mwakilishi kutoka shirika la hifadhi la nyanda za juu kusini Godwell ole meing'ataki kushoto akiwa na waziri kivuli wa maliasili na utalii mbunge Peter Msigwa ambae alikuwa mgeni rasimi jana katika maadhimisho ya Tembo Duniani

Na Francis Godwin Blog,Iringa
KWA mara ya kwanza mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amevunja rekodi ya kuhotubia wananchi wachache kuliko mihadhara mbali mbali aliyopata kuifanya katika uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa .
Uwanja huo ambao ni uwanja wa Histori kwa mbunge Msigwa kupata wasikilizaji wengi jana amejikuta akiambulia patupu baada ya idadi ya watu waliofika kumsikiliza kufika idadi ya chini ya 30 jambo ambalo limezua maswali mengi zaidi.
Pamoja na kuwa mhadhara huo wa leo haukuandaliwa na Chadema bali ulilenga kuadhuimisha siku ya Tembo Duniani ila bado kwa kiasi mvuto wa maadhimisho hayo yamepoteza mwelekeo .
Baadhi ya wadau waliozungumza na mtandao huu wamedai kuwa waandaaji wa maadhimisho hayo ya siku ya Tembo Duniani ndio ambao wamefanya maadhimisho hayo bila kujiandaa na ndio sababu ya wananchi kupuuza kufika uwanjani hapo.
Kwa upande wake mbunge Msigwa alimtaka Rais Jakaya Kikwete kuwachukulia hatua wale wote wanaotajwa kujihusisha na ujangili wa meno ya tembo ambao waziri wa maliasili na utalii amekuwa akieleza umma kuwa watu hao wanajulikana .
Msigwa aliwataka wananchi wa nyanda za juu kusini kufichua majangili wa meno ya tembo ili kuendeleza utalii na kujipatia kipato.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa maadhimisho ya kupinga uuaji wa tembo dunuani ambayo yamefanyika mkoani Iringa yenye kauli mbiu inayosema pinga ujangiri,na kubainisha kuwa utalii bila tembo hakuna utalii.
"Napenda kutoa rai kwa kupitia hadhara hii kumshinikiza Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kwa dhamana aliyopewa kwa kupitia katiba, aweze kuwafikisha mbele ya vyombo vya dola na kuwatendea ipasavyo watuhumiwa wote wa ujangili hasa wa tembo....Natoa shinikizo hili kwa kuwa mara kadhaa, mawaziri wenye dhamana wameendelea kukiri kuwa wanawafahamu majangili mpaka sehemu wanazokaa lakini imeendelea kuwapa muda. Swali la kuuliza, je tunasubiri tembo watoweke ndio tuanze kumtafuta mbaya/mchawi wetu? Ama ndo msemo wa waswahili kuwa 'La kuvunda halina ubani?'"
Msigwa alisema kuwa moja kati ya maazimio katika maadhimisho ya siku ya tembo ni pamoja na kumtaka Raisi kuwachukulia hatua maafisa na watendaji wote wa Serikali na vyombo vya usalama ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakishukiwa na kushutumiwa kwa ushiriki wao hasa katika kulinda ama kusaidia mtandao wa ujangili nchini.
Alisema kuwa Rais Kikwete hana budi kulichukulia jambo hili la ujangili wa tembo kwa uzito mkubwa na kulipa nafasi katika moja ya mambo ya msingi ambayo kama Taifa lazima tuyazungumze bila kificho wala kulinda maslahi ya watu wachache tena kwa uwazi na ukweli kwa kushirikiana na umma wa watanzania.
"Mapambano dhidi ya ujangili na ukatili wa tembo lazima yafanywe kwa dhamira ya dhati na si kwa nia ya kuwapumbaza wananchi huku watu waliopo katika mtandao wa ujangili wakilindwa na kujinufaisha kwa maslahi yao "
Hata hivyo alisema hadi sasa ni dhahiri kuwa ukimya wa Serikali na kigugumizi chake cha kuwachukulia hatua watuhumiwa kunatokana na ubinafsi, uozo na kutojali maslahi ya taifa kwa ujumla.
"...Napenda kuwahakikishia waandaji kuwa , nitaendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda rasilimali hizi muhimu na urithi huu mkubwa wa taifa letu kwa moyo wangu, nafsi yangu,nguvu zangu na akili zangu kwa kushirikiana na watanzania wote kwa ujumla bila kujali tofauti za kiitikadi na misimamo...ningependa kuongea mengi, ila kwa leo napenda kumalizia kwa kuwakumbusha wananchi pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea kutimiza wajibu wake wa kulinda haki za wanyamapori hasa tembo hata pale tunapoona kuwa Serikali inafanya jitihada hafifu katika mambo ya msingi.
kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika la hifadhi la nyanda za juu kusini Godwell ole meing'ataki amesema kuwa Serikali inachangia billion 11 katika kuendeleza miradi ya wananchi kama maji elimu,miradi ya kijamii na na kimazingira ambayo fedha hizo zinatoka katika mfuko wa utalii na maliasili.
Meing'ataki amewaomba wananchi pia kuwafichua wmajangiri wa tembo ili kusaidia watalii waweze kuja nchini na kujipatia kipato ili nchi iweze kuendeleza miradi ya kijamii.
Serikali kwa kutimiza wajibu wake wa kudhibiti biashara haramu ya wanyamapori ni lazima pia mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea kuongeza juhudi zao kuhakikisha kuwa elimu kutolewa kwa umma ili kuongeza nguvu ya pamoja katika masuala ya kulinda wanyamapori.

No comments:

Post a Comment