Baadhi ya washiriki wa shindano la Tusker Project Fame msimu wa sita wakisikiliza kwa makini maelekezo ya watangazaji wa kipindi hicho(hawapo pichani)kutoka kushoto ni mshiriki kutoka Tanzania Hisia, Hope kutoka Burundi na Bior kutoka Sudan ya Kusini
Mmoja wa washiriki kutoka Tanzania aliyeingizwa kikaangoni Angella Karashani(Angel)akimiliki jukwaa katika kipindi cha tatu cha Tusker Project Fame msimu wa sita huku akiimba kibao cha‘Don’t You Remember’ chake Adele Jumapili jijini Nairobi.
Mmoja wa washiriki wanaoiwakilisha vyema Tanzania Elisha Maghiya(Hisia)akimiliki jukwaa katika kipindi cha tatu cha Tusker Project Fame msimu wa sita huku akiimba kibao cha `Here I Stand’ chake Usher Jumapili jijini Nairobi.
28 Oktoba 2013, Ni baada ya vuta nikuvute katika kinyaganyiro
cha shindano la vipaji vya kuimba maarufu kama Tusker Project Fame kipindi cha
tatu ambapo kila mshiriki alikuwa amejinoa vya kutosha ili kuhakikisha
anaendelea kubaki katika mashindano hayo. Wawakilishi wa nchi yetu Angel na Hisia walionekana kufanya
vyema huku Hisia akipagawisha zaidi.
Mashindano yalianza huku kila mmoja akionesha kuwa na shauku
kubwa hasa Bior, Fessy pamoja na Jennifer ambao walinusurika katika hatari ya
kutolewa katika mashindano hayo baada ya kuwa wamerudia nyimbo zao siku ya
jumamosi na kufanikiwa kubaki katika shindano hilo. Mishel kutoka Kenya pamoja
na Under Coverbrothers kutoka Uganda waliaga mashindano hayo siku ya jumamosi.
Angel alimiliki jukwaa mara baada ya Patrick kufungua zoezi
hilo. Akiwa amevalia gauni nyekundu iliyokuwa ikionesha wazi muonekano mzuri
alionao huku ikimstiri vizuri aliimba wimbo wa ‘Don’t You Remember’ wa
Adele. Alifanya vizuri huku
akishangiliwa na mashabiki waliovutiwa
na hisia zake katika kuimba wimbo huo. Majaji walionekana kutoridhirishwa sana na
uimbaji wake wakimtaka aongeza jitihada kwani sauti ya kuimba anayo na anaweza,
kikubwa ni kuongeza bidii.
Hisia nae alionyesha umahiri wake katika kuitumia sauti,
kujiamini na kulimilliki vyema jukwaa baada ya kuutendea haki wimbo wa ‘Here I
Stand’ wa Usher. Kutokana na kulitawala
vyema jukwaa mashabiki walishindwa kujizuia hivyo wakaenda nae sambamba katika
kuimba huku wakimshangilia na kuonesha kuwa hawana upinzani na uimbaji wake.
Majaji nao hawakuwa na lakuongeza zaidi ya kumpongeza huku jaji Hermes
akimpongeza kwa kumwambia kuwa Tanzania inajivunia uwepo wake katika mashindano
haya. Pia mwalimu wa washiriki wa Tusker Project Fame Musyoka alimpogeza sana
kwa kuyazingatia yale yote aliyofundishwa na kumtaka akaze kamba.
Wasanii wengine waliopagawisha ni pamoja na Bior mshiriki
kutoka Sudani ya kusini ambae anapendwa sana na mashabiki na anaweza kulimili
jukwaa vilivyo japo alikuwa katika hatari ya kutolewa na badae kujikomboa. Pia
msanii Patrick aliyingia jukwaani na kibao cha I’m an African in New York’ cha Sting alionekana kuwabamba sana mashabiki na
majaji hivyo kujihakikishia nafasi nzuri katika shindano hilo.
Mwisho wasanii wote walirudi jukwaani kwa pamoja ili kuvuna
walichokipanda. Baada ya maelezo mafupi Jennifer alikuwa ni mshiriki wa kwanza
kuchaguliwa kuwa katika hatari ya kutolewa huku ikiwa ni mara yake ya pili sasa
kuwa katika hatari hiyo baada ya kunusurika katika kipindi kilichopita kwa
kuokolewa na washiriki wenzake. Wa pili
katika hatari hiyo alikuwa Angel mshiriki kutoka Tanzania ambae anahitaji sana
kura zetu watanzania ili kuendelea kubaki katika mashinano hayo kwani uwezo wa
kuimba anao. Wa tatu alikuwa ni Phionah kutoka Rwanda na wa mwisho alikuwa ni
Fessy ambaye pia alirudi katika hatari kwa
mara ya pili sasa.
Kabla ya onesho kuisha Dr Mich alimtambulisha mkurugenzi
mpya wa muziki kwa wiki hii ambae ni jaji Hermes Bariki.
Meneja wa bia ya Tusker Sialouise Shayo kutoka katika
kampuni ya bia ya Serengeti aliwashukuru sana na kuwapongeza washiriki Hisia na
Angel kwa kuendelea kuiwakilisha vyema nchi yetu. Pia alisisitiza sana katika
suala la kumpigia kura kwa wingi Angel kwani ana kipaji kikubwa na anaweza
kusonga mbele kikubwa ni ushirikiano wa Watanzania katika kumuinua. Pia
aliongeza kuwa kampuni hiyo ipo pamoja na watanzania katika kuhakikisha
wanatuletea ushindi wa msimu huu.
Mpigie
kura mshiriki Angel (Tusker 14) kutoka Tanzania ili
aendelee kupeperusha bendere ya nchi yetu ili kumuwezesha kubakia katika
shindano hilo. Usikose kufatilia moja kwa moja kipindi cha Tusker
Project Fame
msimu wa sita kupitia televisheni za
EATV saa 2:00 usiku siku ya Juma mosi na saa 1:30 usiku siku ya
Jumapili, pamoja na televisheni ya ITV kuanzia saa 4:00 usiku Juma
mosi na Jumapili.
Kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako, haiuzwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.
No comments:
Post a Comment