Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd kupitia magazeti yake ya Mwananchi na The Citizen, yalipata fursa pekee ya kumuhoji Rais Maya Graf, kuhusiana na masuala mbalimbali ikiwamo madhumuni ya safari yake, mabilioni hayo, uwazi wa mishahara ya viongozi wa juu serikalini na uhuru wa vyombo vya habari. Mwandishi wetu, Noor Shija alikuwa mmoja wa walioshiriki kufanya mahojiano na kiongozi huyo wa kitaifa na yafuatayo ni mahojiano hayo:
Swali: Nini madhumuni ya safari yako na hii ni mara yako ya kwanza kutembelea Afrika na hasa Tanzania?
Jibu: Hii siyo mara yangu ya
kwanza kutembelea Afrika, mara ya kwanza kuja Afrika ilikuwa mwaka 2011,
nilitembelea nchi ya Senegal. Lakini kwa Tanzania ni mara yangu ya
kwanza na kwa wadhifa wangu wa Rais naruhusiwa kusafiri nje ya nchi.
Na mimi nilichagua Tanzania kwa sababu ya uhusiano
mzuri kati ya Uswisi na Tanzania uliodumu kwa miaka mingi. Kuna raia
wengi wa Uswisi wanaoishi Tanzania, pia tunasaidia miradi mbalimbali ya
maendeleo kama vile hospitali ya Ifakara (Morogoro), ambayo
nimeitembelea.
Pia tunashiriki katika uendelezaji wa miradi
mingine mbalimbali kama vile sekta ya kilimo, makazi na masuala mengine
yanayohusiana na Serikali. Nikiwa Rais wa Bunge ni muhimu kwangu
kuthibitisha fedha tunazosaidia Tanzania kama zinatumika kwa malengo
yaliyokusudiwa.
Swali: Ulikutana na Spika wa Bunge la
Tanzania, Anne Makinda. Mazungumzo yenu yalilenga maeneo gani na nini
matokeo ya mkutano wenu?
Jibu: Kwanza nilifurahi kuonana
na Spika, kwa kuwa sote ni wanawake katika nafasi ya uongozi unaofanana,
mazungumzo yetu yaliegemea sana kuhusu nafasi za wanawake katika
uwakilishi wa uongozi wa kisiasa.
Tulizungumza kuhusu kanuni na taratibu za mabunge yetu, pia tulizungumza kuhusu changamoto tunazokabiliana nazo.
Pia tulizungumza kuhusu idadi ya wanawake ndani ya
Bunge na umuhimu wa wanawake kushika nafasi za uongozi katika sekta ya
elimu, sekta ya uchumi na katika ngazi za juu za uongozi. Hayo ndiyo
tuliyozungumza.
Swali: Nchi yako imekuwa na uhusiano
wa muda mrefu na Afrika, na hasa Tanzania katika masuala ya Bunge,
diplomasia na misaada ya maendeleo. Kwa kifupi unaweza kuelezea uhusiano
wa masuala ya Bunge na hasa katika kubadilishana uzoefu?
Jibu: Tuna uhusiano wa muda mrefu
hasa katika ngazi ya kibunge, tumekuwa tukifanya kazi pamoja katika
masuala ya umoja ya kibunge (Inter-Parliamentary Union-IPU), ambapo
*fanyika Geneva, Uswisi, hivi karibuni Anne Makinda alihudhuria, lakini
hatukubahatika kuonana.
Masuala mengine ni kama vile misaada ya
kimaendeleo ambayo imeimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Uswisi,
mfano miradi iliyopo Dodoma na Ifakara (Morogoro).CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment