Pages

Saturday, October 12, 2013

Rwanda yaondoa watoto jeshini lakini inawaandikisha kwa M23

rwanda ed3f8
Katika kipindi cha miaka 16 iliyopita nchi ya Rwanda imefanikiwa kuondoa kutoka jeshini wanajeshi watoto wapatao 3,000. Lakini wakati juhudi hizi zinaendelea Umoja wa Mataifa unasema Kigali imekuwa ikilisaidia kundi moja la waasi kutoka Congo la M23 kuwaandikisha watoto nchini Rwanda na kuwapeleka kuungana na waasi wa M23 kushiriki katika mapambano Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Katika utaratibu wa kuwatoa watoto jeshi Rwanda kwanza hupeleka wapiganaji wa zamani wa FDLR kwanza kambi ya Mutobo ambako wapiganaji wa zamani wote wanaume na wavulana wanakaa kwa miezi mitatu. Wanajeshi wa zamani watoto kisha wanapelekwa kwenye kituo cha ushauri nasaha ambako wanapatiwa ushauri, dawa, kurudi tena kwenye masomo yao ya msingi na juhudi zinafanywa za kuwatafuta ndugu zao.
Lakini wakati Rwanda inafanya kazi kusaidia watoto kutoka nchini mwake kurudi nyumbani mkuu wa kitengo cha kumlinda mtoto katika Umoja wa Mataifa-MONUSCO mjini Kinshasa, Dee Brillenburg Wurth, anasema Rwanda inaandikisha watoto wengine makusudi na kwa mfumo maalumu ili kuwapeleka kufanya kazi kwa ajili ya kundi la M23 baadhi yao ni watoto wenye umri wa miaka 11. Wakati MONUSCO haiwezi kufanya kazi nje ya Congo, Brillenburg Wurth anasema wana ushahidi kwamba nchi ya Rwanda hivi sasa inaandikisha watoto.
Bi.Wurth anasema kati ya watoto 122 waliohojiwa watoto 37 walikuwa wanyarwanda. Baadhi yao waliandikishwa katika nchi yao, baadhi nchini Congo. Baadhi wanafikiri walipatiwa mafunzo na jeshi la Rwanda na wengine hawakufahamu iwapo walikuwa nchini DRC. "Wengi wao walitekwa nyara, kama ilivyo kawaida kwa makundi yeyote yenye silaha, unakwenda kupora au unahitajika kubeba silaha kutoka sehemu moja kwenda nyingine, unachukua watoto kutoka vijijini na huwapi fursa ya kurudi tena. Watoto wengi takribani wote walianza maisha yao kama watoto wa M23 wakibeba vifaa kutoka mpaka wa Rwanda".
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo anakanusha vikali kwamba Rwanda inaandikisha watoto. "Rekodi zetu katika mfumo wa jeshi ipo wazi. Rwanda haiwezi kuvumilia kuona watoto wanaandikishwa katika makundi yoyote yake yenye silaha, sio tu katika jeshi letu wenyewe."
Mkuu wa MONUSCO alisema mara ghasia huko mashariki mwa Congo zikimalizika na makundi yenye silaha yatokomezwe kisha uandikishaji wanajeshi watoto utamalizika.
Marekani imeweka shinikizo lake yenyewe kwa Rwanda ikisitisha msaada wa kijeshi kwenda Kigali kutokana na shutuma zinazotolewa kwa nchi hiyo kuandikisha kwake wanajeshi watoto. Chanzo: voaswahili

No comments:

Post a Comment