Afisa
Habari Mwandamizi toka Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Bi.
Prisca Ulomi(kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)
kuhusu Uanzishwaji wa Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,
wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo
Jijini Dar Es salaam.Kulia ni Afisa Habari Idara 6ya Habari(MAELEZO)
Hassan Silayo.
Picha na Eliphace Marwa-MAELEZO
Picha na Eliphace Marwa-MAELEZO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
UANZISHWAJI WA TUME YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
TAREHE 3 OKTOBA, 2013
• Mkurugenzi, Idara ya Habari MAELEZO, Bw. Asah Mwambene;
• Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Bi. Zamaradi Kawawa;
• Ndugu Wanahabari;
• Ndugu Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
TAREHE 3 OKTOBA, 2013
• Mkurugenzi, Idara ya Habari MAELEZO, Bw. Asah Mwambene;
• Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Bi. Zamaradi Kawawa;
• Ndugu Wanahabari;
• Ndugu Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Habari za asubuhi.
1.
Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wote mliofika katika mkutano huu
muhimu wenye lengo la kuwaelimisha wananchi na wadau wa Sekta ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kuhusu umuhimu wa kuundwa
kwa Tume ya kitaifa ya kuratibu, kusimamia na kuendeleza TEHAMA nchini.
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni moja kati ya Sekta
zinazokua kwa kasi hapa nchini na duniani kote na imekuwa ikichangia
kikamilifu katika maendeleo ya Taifa na pia imekuwa ikiwezesha sekta
nyingine kukua na kuboresha maisha ya wananchi na huduma za jamii kwa
ujumla. Kutokana na ukuaji wa Sekta hii, jitihada za makusudi
zinahitajika katika kusimamia na kuratibu shughuli za TEHAMA ili nchi
iweze kunufaika zaidi kwani mchango wa sekta hii unaweza kuwa mkubwa
kama TEHAMA na matumizi yake yataratibiwa, kusimamiwa na kuendelezwa
vyema zaidi kuliko hali ilivyo sasa. Katika kuhakikisha masuala ya
TEHAMA nchini yanaratibiwa, kusimamiwa na kuendelezwa vyema, Serikali
iliona ni vema ikaundwa Tume ya TEHAMA (ICT Commission). Uamuzi huu
pamoja na mambo mengine, unatambuliwa na Sera ya Taifa ya TEHAMA ya
mwaka 2003 ambayo pia inaelekeza kuundwa kwa chombo cha TEHAMA ikiwemo
juhudi na program mbalimbali zinazoendelea hapa nchini zinazohitaji
utaratibu wenye ufanisi. Aidha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia inaendelea na taratibu za uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA
ikiwepo juhudi na program mbalimbali zinazoendelea hapa nchini
zinazohitaji uratibu wenye ufanisi. Kwa kutambua mchango wa wadau katika
ukuzaji wa sekta ya Mawasiliano nchini, wadau mbalimbali wa masuala ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wamehusika na kushiriki kikamilifu
kutoa maoni katika hatua zote za uanzishwaji wa Tume hii. Tume hii
inalenga kutambua na kuvutia fursa za uwekezaji katika TEHAMA, kutoa
ushauri, kuendeleza rasilimali watu kitaifa kwenye sekta ya TEHAMA,
kuendeleza program za kitaifa za TEHAMA na kushiriki katika kuendeleza
miundombinu mbalimbali ya TEHAMA yenye sura ya kitaifa kwa kushirikisha
wadau wa sekta zote.
Ndugu Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,
2.
Jitihada za kuanzisha Tume zinalenga kutekeleza Sera ya Taifa ya TEHAMA
pamoja na maazimio mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikiwemo maagizo ya
Mkutano wa Dunia wa Jamii Habari (World Summit on Information Society).
Aidha, jitihada mbalimbali zimefanywa na Serikali katika kuhakikisha
Sekta ya TEHAMA inakua nchini. Miongoni mwa jitihada hizo ni pamoja na
uanzishwaji wa vituo vya Mawasiliano vya Jamii (community telecentres),
ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (National ICT Broadband
Backbone-NICTBB), Uanzishwaji wa Wakala wa Serikali Mtandao, Uanzishwaji
wa Vituo vya Kutunzia kumbukumbu za TEHAMA (Data centres), na Mradi wa
Anwani za Makazi na Simbo za Posta (Physical Adressing System and
Postcode).
Ndugu Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,
3.
Mafanikio katika jitihada hizi yamekabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo
kutokuwepo kwa chombo mahususi kinachoratibu, kusimamia na kuendeleza
TEHAMA nchini. Ni dhahiri kuwa sekta ya Mawasiliano inakuwa kwa kasi
kubwa sana duniani kote na hapa nchini kwetu, na hivyo kufanya baadhi ya
mambo kuwa na changamoto katika utekelezaji wake hususan kutokuwepo na
uratibu wa kitaifa katika miradi na program zenye sura ya kitaifa. Pia,
kukosekana kwa mpango wa Kitaifa wa usimamizi wa kuhakikisha kuwa mifumo
ya TEHAMA inawasiliana na hatimaye kuepuka upotevu wa rasilimali
unaotokana na taasisi mbalimbali kufanya kitu kile kile (duplication of
efforts); Changamoto nyingine ni kutokuwapo na usimamizi, usajili wa
kitaifa wa kuendeleza weledi kwa wataalamu wa TEHAMA (professional
development, registration and certification) na kuhakikisha utoshelevu
wa rasilimali watu utakaokidhi mahitaji ya maendeleo ya TEHAMA;
Kutokuwepo chombo mahususi chenye majukumu ya kisheria.
Ndugu Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,
4. Tume
hii inatarajia kuondoa changamoto hizo tajwa hapo juu na kujenga mfumo
utakaowezesha uwekezaji wa kushirikisha sekta binafsi katika ujenzi wa
miundombinu ya mawasiliano na TEHAMA yenye sura ya kitaifa; Kuwepo mfumo
utakaowezesha wabunifu na wajasiriamali kuendeleza sekta ya TEHAMA; na
kuweka utaratibu na miongozo ya namna bora ya kuhifadhi vifaa chakavu
vya TEHAMA (e-waste management).
Ndugu Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,
5. Tume
ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano itasaidia kukuza uchumi wa Taifa
kutokana na kukua kwa sekta ya TEHAMA na kuchochea uzalishaji, ukuaji wa
sekta zingine kiuchumi na usambazaji wa huduma za jamii; kuwa na taifa
la jamii Habari, lenye wataalam wanaotambulika kitaifa na kimataifa, na
wajasiriamali katika Nyanja mbalimbali za TEHAMA kuendana na kasi ya
ukuaji wa teknolojia duniani; kuwa na uhakika wa usalama katika matumizi
ya TEHAMA na kuwepo na mfumo unaoainisha na kuendeleza uwekezaji katika
sekta ya TEHAMA kitaifa.
Ndugu Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,
6. Kwa niaba ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wadau na wananchi wote wanaoshiriki kwa njia moja au nyingine katika uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA nchini.
Asanteni kwa kunisikiliza.
6. Kwa niaba ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wadau na wananchi wote wanaoshiriki kwa njia moja au nyingine katika uanzishwaji wa Tume ya TEHAMA nchini.
Asanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na;
Prisca J. Ulomi
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
No comments:
Post a Comment