Untitled
Bw. Benedict Mashauri  akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kutangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Maswa Magharibi kupitia tiketi ya Chadema.(picha Daniel Makaka, Sengerema Mwanza).

Na.Daniel Makaka Sengerema.
Mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi Mh. John  Shibuda, ametumiwa  salamu na vijana wapenda maendeleo wa jimbo hilo ajiandae  kuachia madaraka katika jimbo hilo kwa hiyari kwani akifanya hivyo atakuwa ametunza heshima yake, asisubiri kuaibika 2015.
Salamu hizo zimetumwa na kijana mpenda maendeleo anayejipanga kumng’oa katika jimbo hilo Bw. Benedict Mashauri  Magessa baada ya kuombwa na Wazee pamoja na wananchi wa jimbo agombee ubunge jimboni humo kupitia tiketi ya Chadema.
Bw. Mashauri ameyasema hayo alipokuwa akiongea na wandishi wa habari hivi karibuni juu ya maamuzi ya kugombea ubunge katika jimbo hilo la Maswa Magharibi .
Ameongeza kuwa kutangaza nia  ni haki ya kila mmoja hivyo hawezi kuwaangusha wananchi waliomuomba na kuwataka wamuunge mkono ili awe Mbunge wa Jimbo hilo 2015.
11
Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi (CHADEMA), Mhe John Shibuda.