WILAYA YA ILEJE – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 01.10.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHAIZUBA WILAYA YA ILEJE MKOA WA MBEYA. SIKWITA D/O NAMWOVE, MIAKA 70, MLAMBYA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IZUBA ALIUAWA KWA KUKATWA PANGA SHINGONI NA MOHAMED S/O MWAMAHONJE, MIAKA 36, MKULIMA, MLAMBYA, MKAZI WA KIJIJI CHA IZUBA. MBINU NI KUMVIZIA MAREHEMU AKIWA JIKONI NYUMBANI KWAKE NA KUMUUA. CHANZO NI IMANI ZA KISHIRIKINA BAADA YA MTUHUMIWA KUMTUHUMU MAREHEMU KUWA ANAMLOGA. MWILI
WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI WA SERIKALI NA KUKABIDHIWA
NDUGU KWA MAZISHI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUSADIKI IMANI POTOFU ZA
KISHIRIKINA KWANI ZINALETA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 01.10.2013 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA ITIJI JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA MOSES S/O SAID MIAKA 17, KYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA ITIJI AKIWA NA BHANGI KETE 14 SAWA NA UZITO WA GRAM 70. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KATIKA KIBANDA CHAKE CHA BIASHARA YA KUUZA SIGARA.
MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment