Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, October 3, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI“PRESS RELEASE” TAREHE 02. 10. 2013.

DSC00260
WILAYA YA  MBEYA MJINI   -         WATUHUMIWA  105 WANASHIKILIWA NA JESHI LA
                                                              POLISI MKOA  WA MBEYA KUTOKANA KWA 
                                                                     TUHUMA YA  KUFANYAVURUGU NA   UHARIBIFU
                                                                WA MALI.
  • MNAMO TAREHE 02.10.2013 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA MAENEO YA MWANJELWA, SOWETO, MAMA JOHN NA ILOMBA KUNDI LA VIJANA WAKOROFI NA WASIO  TAYARI KUTII SHERIA WALISHINIKIZA WAFANYABIASHA KUFUNGA BIASHARA ZAO NA KISHA KUFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/IRINGA  NA BARABARA ZA MITAA KWA KUWEKA MAWE MAKUBWA,  MAGOGO, KUCHOMA MOTO MATAIRI NA KURUSHA OVYO MAWE KWA ASKARI POLISI HALI ILIYOSABABISHA USUMBUFU KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA NA WANANCHI WA JIJI LA MBEYA KWA UJUMLA. 
  • KUFUATIA VURUGU HIZO JESHI LA POLISI LILIKABILIANA NAZO NA KUFANIKIWA KUREJESHA HALI YA AMANI.
  • CHANZO CHA TUKIO HILI NI WAHALIFU/WAFANYAFUJO KUTUMIA KIVULI CHA MALALAMIKO/MANUNG’UNIKO YA WAFANYABIASHARA KWENYE ENEO LA KODI HUSUSANI CHANGAMOTO KWA WAFANYABIASHARAWADOGOWADOGO KUWA BEI YA MASHINE YA KI-ELEKRONIKI NI GHALI  KIASI CHA TSH 800,000/= HIVYO WAO KUSHINDWA KUNUNUA. 
  • KABLA YA VURUGU HIZO TAREHE 01.10.2013 WAFANYABIASHARA ZAIDI YA 300 WALIPATA FURSA YA KUKUTANA NA MKUU WA MKOA MHE ABBAS KANDORO WAKATI  WAFANYABIASHARA HAO WALIPOKUWA NA SEMINA ILIYOANDALIWA NA MAOFISA WA MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA MBEYA. KATIKA KIKAO HICHO WALIMUELEZA MKUU WA MKOA MANUNG’UNIKO WALIYOKUWA NAYO IKIWA NI PAMOJA NA BEI YA MASHINE YA ELEKRONIKI INAYOFANYA KAZI YA KUTOA RISITI KWA WATEJA NA KUWEKA KUMBUKUMBU. 
  • JUMLA YA WATUHUMIWA 105  WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA MIONGONI MWAO WANAUME 103 NA WANAWAKE 2 KWA MAHOJIANO NA WATAKAOBAINIKA KUHUSIKA KATIKA TUKIO HILI HATUA ZA KISHERIA IKIWA NI PAMOJA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI ZITAFUATA.
  • HAKUNA MADHARA MAKUBWA KWA BINADAMU AU MALI YALIYOTOKEA ISIPOKUWA UHARIBIFU WA KUCHOMA BARABARA. 
  •  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI   ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA  WANANCHI NA WAKAZI WA MBEYA KUTOICHEZEA AMANI ILIYOPO KWANI  GHARAMA YA KUIRUDISHA NI KUBWA. AIDHA ANATOA RAI KWA WAFANYABIASHARA  KUENDELEA KUTAFUTA UFUMBUZI WA MATATIZO YAO KWA NJIA YA KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO KWA KUJENGA HOJA KWA MISINGI YA KUTIISHERIA  ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. PIA ANAENDELEA KUTOA RAI  YA KUENDELEA KUWAFICHUA WAHALIFU WAKIWEMO WAFANYA FUJO,VURUGU NA KUKATAA KUWAUNGA MKONO KATIKA MAOVU. 
       
Signed by 
 [ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment