POLISI MKOA WA MBEYA KUTOKANA KWA
TUHUMA YA KUFANYAVURUGU NA UHARIBIFU
WA MALI.
- MNAMO TAREHE 02.10.2013 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA MAENEO YA MWANJELWA, SOWETO, MAMA JOHN NA ILOMBA KUNDI LA VIJANA WAKOROFI NA WASIO TAYARI KUTII SHERIA WALISHINIKIZA WAFANYABIASHA KUFUNGA BIASHARA ZAO NA KISHA KUFUNGA BARABARA KUU YA MBEYA/IRINGA NA BARABARA ZA MITAA KWA KUWEKA MAWE MAKUBWA, MAGOGO, KUCHOMA MOTO MATAIRI NA KURUSHA OVYO MAWE KWA ASKARI POLISI HALI ILIYOSABABISHA USUMBUFU KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA NA WANANCHI WA JIJI LA MBEYA KWA UJUMLA.
- KUFUATIA VURUGU HIZO JESHI LA POLISI LILIKABILIANA NAZO NA KUFANIKIWA KUREJESHA HALI YA AMANI.
- CHANZO CHA TUKIO HILI NI WAHALIFU/WAFANYAFUJO KUTUMIA KIVULI CHA MALALAMIKO/MANUNG’UNIKO YA WAFANYABIASHARA KWENYE ENEO LA KODI HUSUSANI CHANGAMOTO KWA WAFANYABIASHARAWADOGOWADOGO KUWA BEI YA MASHINE YA KI-ELEKRONIKI NI GHALI KIASI CHA TSH 800,000/= HIVYO WAO KUSHINDWA KUNUNUA.
- KABLA YA VURUGU HIZO TAREHE 01.10.2013 WAFANYABIASHARA ZAIDI YA 300 WALIPATA FURSA YA KUKUTANA NA MKUU WA MKOA MHE ABBAS KANDORO WAKATI WAFANYABIASHARA HAO WALIPOKUWA NA SEMINA ILIYOANDALIWA NA MAOFISA WA MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA MBEYA. KATIKA KIKAO HICHO WALIMUELEZA MKUU WA MKOA MANUNG’UNIKO WALIYOKUWA NAYO IKIWA NI PAMOJA NA BEI YA MASHINE YA ELEKRONIKI INAYOFANYA KAZI YA KUTOA RISITI KWA WATEJA NA KUWEKA KUMBUKUMBU.
- JUMLA YA WATUHUMIWA 105 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA MIONGONI MWAO WANAUME 103 NA WANAWAKE 2 KWA MAHOJIANO NA WATAKAOBAINIKA KUHUSIKA KATIKA TUKIO HILI HATUA ZA KISHERIA IKIWA NI PAMOJA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI ZITAFUATA.
- HAKUNA MADHARA MAKUBWA KWA BINADAMU AU MALI YALIYOTOKEA ISIPOKUWA UHARIBIFU WA KUCHOMA BARABARA.
- KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI NA WAKAZI WA MBEYA KUTOICHEZEA AMANI ILIYOPO KWANI GHARAMA YA KUIRUDISHA NI KUBWA. AIDHA ANATOA RAI KWA WAFANYABIASHARA KUENDELEA KUTAFUTA UFUMBUZI WA MATATIZO YAO KWA NJIA YA KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO KWA KUJENGA HOJA KWA MISINGI YA KUTIISHERIA ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. PIA ANAENDELEA KUTOA RAI YA KUENDELEA KUWAFICHUA WAHALIFU WAKIWEMO WAFANYA FUJO,VURUGU NA KUKATAA KUWAUNGA MKONO KATIKA MAOVU.
Signed by
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment