Mshambuliaji huyo wa Manchester United aliingia katika mchezo huo wa kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil, akiwa ana mabao 38 katika mechi 78 za Orange, na wenyeji hawakuwa na presha kwa kuwa walikwishajihakikishia tiketi ya Brazil Septemba mwakani.
Van Persie alifunga dakika ya 16 kabla ya Kevin Strootman na Jeremain Lens kuongeza.
Nahodha wa The Orange akafikia rekodi ya mabao 40 ya Patrick Kluivert karibu na mapumziko na akashangilia kwa kumkumbatia Kluivert, ambaye ni mmoja wa wasaidizi wa Louis van Gaal katika timu hiyo.
Van Persie akavunja rekodi hiyo kwa bao la dakika ya 53 baada ya kazi nzuri ya Arjen Robben -- ambaye pia alimpa van Persie pasi ya bao la pili kabla ya kumpisha Dirk Kuyt dakika ya 61, Uholanzi wakiibuka na ushindi mnono wa mabao 8-1.
Mabao mengine ya Uholanzi yamefungwa na Strootman dakika ya 25, Jens dakika ya 38, Devecseri akajifunga dakika ya 65, Van der Vaart dakika ya 86 na Robben dakika ya 90, wakati la Hungary lilifungwa na Dzsudzsak kwa penalti dakika ya 47.
Katika mchezo mwingine, bao pekee la Andriy Yarmolenko dakika ya 64 limeipa Ukraine ushindi wa 1-0 dhidi ya Poland na kufufua matumaini ya kucheza Kombe la Dunia.
Nayo Ubelgiji imejikatia tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2002 baada ya mshambuliaji anayecheza kwa mkopo Everton kutoka Chelsea, Romelu Lukaku kufunga mabao mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Croatia.
Matokeo hayo yanamaanisha vinara hao wa Kundi A, Ubelgiji hawawezi kukamatwa kwa pointi zao 25 walizovuna kwenye mechi tisa wakiwa wamebakiza mechi moja nyumbani na Wales Jumanne.
Kiungo wa zamani wa Liverpool, Alberto Aquilani alifunga bao la kusawazisha dakika za majeruhi Italia ikitoa sare ya 2-2 na Denmark katika mchezo wa Kundi B.
Mshambuliaji wa Arsenal, Nicklas Bendtner alifunga mabao mawili na kuwafanya waongoze 2-1, lakini ambayo tayari imekwishafuzu ilipata mabao yake kupitia kwa Daniel Osvaldo na Aquilanina kuiongezea ugumu Denmark wa kwenda Brazil. Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment