Mtoto aliyefariki |
Mtoto
Matrida Michael mwenye umri wa miaka 9, mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ally,
wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, amefariki dunia katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili Oktoba 23, mwaka huu kufuatia majeraha ya moto
aliyoyapata.
Marehemu
Matrida na watoto wenzake wawili, Tatu Mapunda (9) na Flora Mapunda
(7), waliungua moto Oktoba 16, mwaka huu saa tano usiku wakiwa wamelala
baada ya chumba chao kulipuliwa kwa petroli na mtu anayedaiwa kwa ni
Brighton Mnamwa.
Inadaiwa
kwamba chanzo cha Mnamwa kuamua kulipua watoto hao ni ugomvi baina yake
na mkewe Janeth Lwena, waliyekuwa katika mzozo wa kumgombea mtoto wao
wa miaka mitatu aitwaye Tulizo.
Watoto ambao wako hoi |
Mama
mdogo wa marehemu Mary Ivo ambaye alikuwepo msibani hapo, alisema
kwamba dada yake yupo Muhimbili anawauguza majeruhi wawili waliobakia na
kwamba wakati wa ugomvi wao, mke alimzidia nguvu mumewe.
Aidha
aliendelea kueleza kwamba baada ya mke kumzidi nguvu, mume alizusha
ugomvi mkubwa huku akitishia kumuua kwa panga, hata hivyo mke
alimdhibiti.
‘Baadaye
mume huyo inadaiwa kwa aliondoka hapo nyumbani na haikujulikana
alikoenda, ndipo mke alienda chumba cha jirani na kumuomba Matrida
abakie na watoto pale chumbani akatoe taarifa polisi lakini mtoto
aliyekua akigombewa alienda naye kituoni,’ alisema mama mdogo.
Habari
zinasema kwamba yule mume alienda kituo cha mafuta kununua petroli ili
aweze kuwatekezeza wote, lakini hakujua kama mkewe pamoja na mtoto
aliyekua akigombewa hawakuwepo.
Taarifa
zaidi zinaeleza kwamba baada ya mume huyo kurudi, alimimina mafuta hayo
katika chumba hicho kisha kukilipua wakati watoto hao watatu wakiwa
katika usingizi na wananchi walipojitokeza walikuta chumba kikiteketea
huku sauti ya watoto ikisikika wakiomba msaada.
Wananchi
waliokuwepo kwenye eneo la tukio walisema kwamba walipatwa na uchungu
hivyo walijitosa kuuzima moto ule na kuwaokoa watoto hao watatu huku
wakiwa wameungua vibaya, waliwakimbiza Hospitali ya Temeke na kutokana
na hali yao kuwa mbaya walipelekwa Muhimbili ambapo Matrida alifariki
dunia.
Naye
Michael Melkiori Kess, baba wa marehemu alisema kwamba amesikitishwa na
kitendo hicho na amedai ni cha kinyama hivyo ameiomba dola kumsaka mtu
huyo hatari kwani huko aliko kwa sasa bado anaweza kusababisha majanga
megine.
Mwenyekiti
wa serikali ya mtaa wa Mtoni Sabasaba, Mwita Mang’ana alisema kwa
kitendo hicho ni cha kinyama kwani amesababisha kujeruhi watoto wasiokua
na hatia na amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi
kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anapatikana .
Naye
Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kusema kwamba msako wa kumtafuta mtuhumiwa unaendelea
sambamba na uchunguzi wa tukio.
No comments:
Post a Comment