Timu
ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa
Umma ”Kombani queens” ikifanya mazoezi mepesi kabla ya kuingia uwanjani
kupambana na TAMISEMI katika mashindano ya SHIMIWI Kiwanja cha Jamhuri
mjini Dodoma hizi ni taswira za timu ya mpira wa Pete ya Utumishi
“Kombani Queens” ilipoingia fainali kwa kuikung’uta TAMISEMI katika
michezo ya SHIMIWI inayoendelea. Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma ‘Kombani queens” imeshinda mpambnano huo kwa goli 38-28 na
kuingia nusu fainali.
Timu ya mpira wa Pete ya TAMISEMI ikifanya mazoezi kabla ya kupambana
wenzao wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma “Kombani
Queens” . Timu
ya mpira wa Pete ya TAMISEMI ikisalimiana na timu ya Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma “Kombani Queens” kuashiria mwanzo wa
mpambano wao wa Mpira wa Pete kuwania kuingia nusu Fainali za SHIMIWI. Mchezaji
wa timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma “Kombani queens” Monica Aloyce (GK) (aliyeruka juu) akiondoa
hatari kutoka kwa wachezaji wa timu ya TAMISEMI wakati wa mpambano
dhidi ya timu hizo. Mchezaji
wa timu ya mpira wa Pete ya TAMISEMI Defroza Otilia (GA) akijaribu
kutoa pasi wakati wa mpambano na Utumishi mjini Dodoma, mbele yake
akikabwa na mchezaji wa Utumishi Monica Aloyce (GK) . Mchezaji
wa timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma ”Kombani queens” Elizabeth Fussi (C) akitoa pasi wakati wa mpambano
dhidi ya TAMISEMI katika mashindano ya SHIMIWI mjini Dodoma. Mbele
yake ni mchezaji wa TAMISEMI Imelda Hango (C) akijaribu kumzuia .
No comments:
Post a Comment