KATIKA
hali inayoonyesha Haki haiwezi kupatikana pasipo kuandamana,zaidi ya
wanafunzi 500
kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari Manispaa ya Musoma
wamefanya maandamano hadi kituo cha polisi mjini Musoma na baadae kwenda
nyumbani kwa mkuu wa Mkoa wa Mara kwa kile walichokidai kutapeliwa na
mtu wasiye mjua kwa kushirikiana na walimu.
Wanafunzi
hao walifanya maandamano mwishini mwa wiki baada ya mtu mmoja
wasiyemfahamu kwa jina kupita
mashuleni na kuonana na walimu kisha kueleza kutaka kuwafanyisha
wanafunzi mitihani ya taaruma pamoja na michezo na kupewa zawadi
mbalimbali kwa washindi.
Wakizungumza
na Mwandishi wa Blog hii nje ya makazi ya mkuu wa Mkoa walipokwenda kutaka kueleza
matatizo yao,wanafunzi hao ambao walianzia kituo cha polisi na kufukuzwa
walidai walipewa fomu
kwa kununua kwa shilingi
elfu moja na elfu moja mia tano lakini yale waliyoahidiwa kufanyiwa
hawakufanyiwa.
Mmoja
wa wanafunzi hao aliyejitambulisha kwa jina la Leah Sospeter wa shule
ya msingi Kamnyonge 'B',alisema mtu huyo baada ya kufika shuleni
alionana na walimu kisha kupita kila darasa na kudai atawapa mitihani ya
kuwajengea uwezo na kufanya
mashindano mbalimbali ambapo
washindi wangezawadiwa 'Laptop',baiskel,madaftari makubwa lakini
hawakuviona.
"Sisi
hatuwezi kukubali kutapeliwa wazazi wetu wameangaika
kutupa pesa kwa lengo la kufanyishwa mitihani na michezo tunafika
uwanjani hakuna cha mitihani wala michezo na uwanja umefungwa hatukubali
tunataka turudishiwe fedha zetu.
Wanafunzi hao walidai baada ya kuona wanazurumiwa haki yao walikwenda hadi kituo cha polisi musoma ili kuomba msaada wa kukamatwa kwa watu hao lakini waliambuliwa kufukuzwa na kuchukua maamuzi ya kwenda nyumbani kwa mkuu wa Mkoa baada ya kukuta ofisi yake imefungwa.
Baada ya kukusanyika nje ya makazi ya mkuu wa Mkoa na kufunga barabara kwa kuweka mawe wakitaka wamuone ili waeleza kilichowapeleka kwake,askari wa jeshi la polisi walifika katika eneo hilo na kuwatawanya wanafunzi hao ambapo walitawanyika na kupaza sauti tusipopewa haki yetu itatokea kama Soweto.
Kutokana na sakata hilo blog hii lilifatilia katika ofisi ya Utamaduni na michezo ili kufahamu kama wanalijua suala hilo na Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Musoma Reuben Ruhende alikili ofisi yao ilitoa kibali cha kufanyika kwa mashindano hayo ambapo waombaji walijitambulisha kama watu wanaosaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu lakini hawakutekeleza kile walichokiombea kibali.
Alisema watu hao baada ya kuwapa kibali walifanya udanganyifu kwa kupita mashuleni na kuwachangisha wanafunzi fedha kwa maelezo ambayo hayakuwepo kwenye kibali chao na waliporigundua suala hilo walilitaarifu jeshi la polisi na kufanikiwa kukamatwa na wanashikiliwa na jeshi la polisi.
"Ni kweli Afisa Michezo alitoa kibali lakini waandaji wamefanya udanganyifu na ndio maana tulichukua hatua ya kulifikisha suala hilo kwenye vyombo vya dola naamini kwa nafasi yao watalifanyia kazi na haki kwa wanafunzi hao itapatikana,"alisema Ruhende.
HABARI NA SHOMMI BINDA BLOG
No comments:
Post a Comment